Waziri Mkuu wa
zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba alihutubia katika mdahalo huo.
Jaji Warioba, ambaye alikuwa msemaji mkuu kwenye
mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alikuwa
akihitimisha hotuba yakle aliyoianza saa 9:15 alasiri, kwa kuhoji kuhusu
watu wanaotumia vibaya jina la Mwalimu Nyerere kupitisha hoja zao
katika misingi isiyokubalika.
Vurugu hizo zilidumu kwa takriban dakika 45 ndani ya ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Blue Pearl, Ubungo lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wasaidizi wa waziri huyo mkuu wa zamani, walimtoa ukumbini dakika 30 baada ya sakata hilo kuanza, hali iliyowapa nafasi vijana hao walionekana kujiandaa kufanya vurugu, kumsogelea na kumpiga.
Baadhi ya watu walionekana kumzonga Jaji Warioba
ambaye alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ni pamoja na
aliyekuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Paul Makonda.
Baada ya tukio hilo, polisi waliokuwa na silaha na wakiwa wamevalia nguo za kiraia walimtoa Jaji Warioba ukumbini. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz