Jaji Joseph Warioba akitoa mada.
Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa, Jaji
Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi
wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam leo.
Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano
wakiwa na mabango yaliyokuwa yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa
tumeipokea tunaiunga mkono’.
Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili
asipate madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa
kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani.
Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa
mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili
Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole
akimzuia mmoja wa vijana aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa
vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekeza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku
(katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara baada ya
kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa. Mdahalo huo
uliandalia na taasisi hiyo.
Vijana wakiwa na mabango.
Mabango yakiwa juu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Vujo zinaanza.
Mmoja wa vijana waliokuwa wakitoa maneno ya kashfa kwa Jaji Warioba akiwanyooshea vidole viongozi wa meza Kuu.
Baadhi ya viti vilivyovujwa.
Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu.
Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi.
Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya
jengo la Ubungo Plaza ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa
ulikuwa ukifanyika.
Wananchi walikuwa nje ya jengo la Ubungo Plaza wakimshangilia Jaji
Warioba wakati akitoka katika ukumbi wa mdahalo huku wakimuita 'Rais
Rais'.
Polisi na watu wengine wakijaribu kumtuliza jaji Warioba baada ya
kupigwa chupa na Makonda kwenye mdahalo wa katiba uliofanyika leo na
baadae kuvunjika kutokana na vurugu hizo.
Jaji Wariba akitulizwa na baadhi ya watu na polisi aliyekuwepo
hapo kwenye mdahalo wa katiba uliofanyika leo Jumapili Novemba 2, 2014
jijini Dar.
Watu wakipata na mshangao wakijiuliza maswali mengi yasikua na majibu
Palikua patashika nguo chanika. Picha na Francis Dande.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment