KUNA maswali tena? Ndoa ya staa kiwango cha juu Bongo, Irene Uwoya na mumewe Hamad Ndikumana 'Kataut' anayeng'ara katika kabumbu akikipiga pande za Rwanda imerejewa na uhai tena..
Wednesday, April 03, 2013
BREAKING NEWzzzzzzzzzzzzzzz!!!! MPAKA WA TUNDUMA MBEYA WAFUNGWA KWA MUDA POLISI WATUMIA MABOMU
kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman
Taarifa kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai kuwa hali si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa vurugu kubwa zinazodaiwa kusababisha na masuala ya kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam . Mwandishi kutoka Tunduma mkoani Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa vurugu hizo zimeanza majira ya saa nne asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa viongozi wa dini ya kikristo Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa wilaya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa pasaka.
PINDA AFUNGA MACHIMBO YA MORAMU
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyepoteza maisha kutokana na kuporomoka kwa udongo katika machimbo ya Moramu yaliyopo eneo la Moshono, Arusha.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana alitangaza kuyafunga rasmi machimbo ya moramu eneo la Moshono, Arusha hadi Serikali itakapoweka utaratibu mzuri wa shughuli mbalimbali za uchimbaji katika eneo hilo.
Hatua
hiyo ya Pinda imetokana na ajali ya watu 14 waliopoteza maisha baada ya
kufukiwa na kifusi juzi, wakati wengine wawili walijeruhiwa kwenye
ajali hiyo iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na mvua zinazonyesha jijini
Arusha.
Pinda
alitoa agizo hilo alipotembelea eneo hilo pamoja na kuwajulia hali
majeruhi wawili waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mt Meru
CHANZO:MWANANHI.
LOWASSA AMTOA KAFARA PINDA
WABUNGE WAUNGANISHA NGUVU KUTAKA KUMSULUBU BUNGENI
RIPOTI
ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa mwaka
2006 kuchunguza ujenzi wa maghorofa katika Jiji la Dar es Salaam,
imemweka mahala pabaya na inaweza kumtoa kafara, Waziri Mkuu wa sasa,
Mizengo Pinda, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.
Pinda
anatolewa kafara katika sakata la jengo la ghorofa 16 lililoporomoka
katikati ya Jiji la Dar es Salaam wiki iliyopita na kusababisha vifo
vya zaidi ya watu 40.
Kutokana
na janga hilo, Pinda analalamikiwa kukalia ripoti ya Tume ya Lowassa
ambayo ilikuja na mapendekezo ya kukabiliana na maghorofa yaliyojengwa
chini ya kiwango.
SUMATRA YATANGAZA KUPANDA KWA NAULI ZA MABASI YA MASAFA MAREFU NA DALADALA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM
Kaimu
Mkurugenzi wa SUMATRA Athman Kilima akizungumza na waandishi wa habari
leo katika makao makuu ya taasisi hiyo wakati akitangaza kupanda kwa
viwango vya nauli ya mabasi ya mikoani na Daladala.
………………………………………………………………..
Mamlaka
ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha
mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa
mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada
ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama
msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata
kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza
kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.
Subscribe to:
Posts (Atom)