Friday, March 29, 2013
Picha za scenes za movie ya mwisho ya Kanumba ‘Love and Power’
April 7, 2012 ni
siku Steven Kanumba aliyofariki katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu
kifo chake watanzania kutoka sehemu mbalimbali watakutana kwenye tamasha
la bure pale Leaders club kwa lengo la kumuenzi na kuangalia yale
aliyofanya katika enzi za uhai wake pamoja na uzinduzi wa filamu yake ya
mwisho, Love and Power. Hizi ni baadhi ya picha kwenye filamu hiyo.
P FUNK AMCHANA MAKAVU MSANII NAY WA MITEGO
Producer maarufu bongo na mmiliki wa studio za
bongo record P funk Majan ametoa makavu kwa watu wanaochonga kuhusu
maendeleo yake husasani wale wote ambao wanapiga majungu kuwa mkali
huyo amepotezwa na vijana wadogo kwenye soko la mziki bongo. “Kuna watoto wadogo siku hizi wanakurupuka wanajiona wao baabkubwa juzi kati nikiwa kwenye club moja naskia kiproducer kinachonga kuhusu mimi kenyewe kana sijui nyimbo moja au tatu zimehit mimi nina yimbo zaidi ya 100 ambazo zimehit na hadi akina Mhe Mkapa enzi hizo, wametukubali we utaniambia nini” P funk alifunguka. Majani amefunguka kuwa kuna watu wanamtafuta chuki ili kumpachika skendo akitolea mfano msanii wa kizazi kipya Ney wa Mitego kuwa haelewi kitendo cha rapper huyo kumtukana kwenye nyimbo yake kulikua na lengo gani kwasababu msanii huyo hamkaribii hata kidogo kwa level zake. |
JACK PENTZEL ALONGA KUHUSU KUOLEWA KWAKE
MSANII wa bongo movie 'star 'wa bongo
asiyekauka vituko' Jackline Pentzel a.k.a Jack wa Chuzi ameibuka na
kuwataka mashabiki wake kuamini ameolewa na hajakurupuka kufanya
maamuzi hayo kwani ni jambo ambalo alikuwa akilifikiria kila wakati Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni Jack alisema kuwa anawataka mashabiki kuamini na kutowasikiliza watu wengine wanaotoa maneno ya uzushi juu yake kuwa maamuzi ya kuolewa ameyapanga na ameolewa na mwanaume wake wa siku nyingi hivyo anaamini anachokifanya ni sahihi kwake Alisema kuwa watambue mwanaume aliolewa naye si mume wa mtu bali ni mchumba wake wa muda mrefu na walikuwa wakiishi pamoja kbala ya kuoa na ndipo maamuzi ya kufunga ndoa yalipokuja kwa kutotaka kuendelea kufanya uzinifu wakati uwezo wa kufunga ndoa walikuwa wanao "Mimi nawashangaa kwani kuolewa ni kitu gani cha ajabu mpaka watu wasiamini mimi kufunga ndoa nimeamua kuolewa kwa sababu nampenda mwanaume wangu na nilikuwa naishi naye kwa kalibu hivyo tunajuana vizuri sijakulupuka" alisema Pentzel Akizungumzia sababu za kutotangaza harusi yake alisema ameamua kutofanya hivyo ili kuepusha maneno na vizuizi vya ndoa yake ambavyo vingeweza kuibuka na kupoteza mawazo ya mumewake huyo Alisema kuwa hakutaka hali hiyo itokee ndio maana akaamua kufanya iwe siri na ya kushutika ili wambaya wake wakose nafasi ya kufanya jambo lolote baya na kwa sasa baada ya harusi hiyo ndio vikao kwa ajili ya kufanya sherehe hiyo vinapangwa |
PICHA ZAIDI YA HALI ILIVYO SASA KWENYE JENGO LA GHOROFA LILILOANGUKA KATIKATI YA JIJI, DAR
Ni
moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili
kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi
ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa
wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea
mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.
BEAKING NEEEEEWZZZZZZZZ!!!!! GHOROFA LIMEANGUKA MITAA YA ILIGANDI K/KOO
Mpaka
sasa watu watu 12 wameshapoteza maisha,limedondokea msikiti wa SHIA.
Mpaka sasa eneo la tukio
kuna mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na meya,Mmiliki wa jengo hilo bado
hajajulikana.Ndani ya jengo hilo kulikuwa na watu wasio pungua 60
wakiendelea na ujenzi.Watu zaidi ya 14mpaka sasa wameshakimbizwa
hospitali. Tutaendelea kuwajulisha zaidi.
UZINDUZI WA TAWI LA YANGA MAREKANI
TUNAPENDA KUWATANGAZIA RASMI MASHABIKI, WADAU NA WAPENZI WOTE WA TIMU YETU YA SOCCER YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB MLIOPO MAREKANI KUWA TUNAZINDUA RASMI TAWI LETU HAPA MAREKANI LITAKALO JULIKANA KAMA YOUNG AFRICANS FAMILY USA. TUNAOMBA UKIPATA TANGAZO HILI MWARIFU NA MWENZIO.
TAREHE: JUMAMOSI 03/30/2013
MAHALI: KILIMANJARO PASSION RESTAURANT
ADDRESS: 2310 PRICE AVENUE, WHEATON,MD 20902
MUDA: 4:00 PM
KWA MAWASILIANO:
ALEX KASSUWI : TEL :301 305 9685
YOUNG AFRICANS "DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"
SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA LAMSHUSHIA PONGEZI WEMA SEPETU..
SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF)
limempongeza msanii wa kike Wema Sepetu kwa moyo wa upendo aliouonyesha
kwa msanii mwenzie Kajala Masanja kwa kumlipia faini ya sh. milioni 13
alizotozwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kupatikana na
hatia katika kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa inamkabili mahakamani
hapo
Akizungumza kwa niaba ya viongozi
wengine rais wa shirikisho hilo Simon Mwakifwamba alisema kuwa imani na
moyo wa upendo aliokuwa nao msanii Wema ndio uliomsukuma kumlipia
kiwango hicho cha fedha bila ya kujiuliza mara mbili kitendo hiko
kimeonyesha jinsi gani wanavyohitaji kushirikiana katika matatizo.
LEO NI IJUMAA KUU
INAPOFIKA
saa
tisa alasiri, siku kama ya leo, maarufu kama Ijumaa Kuu, katika nyumba
za
ibada za Kikristo, kimya hutanda, mishumaa huzimwa na kuashiria kuwa ni
siku ya
majonzi.
Ijumaa
Kuu ni siku ambayo Wakristo duniani kote hukumbuka mateso aliyoyapata
Yesu
baada ya kusulubishwa msalabani yapata zaidi ya miaka elfu mbili
iliyopita.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeipa thamani siku hii kwa
kuitangaza
kuwa ya mapunziko.
Siku
hii huadhimishwa kwa ibada inayoambatana na kusoma mistari ya Biblia
inayoelezea undani wa matukio yaliyosababisha kusulubiwa kwa Yesu
Kristo.
FILAMU YA SISTER MARRY KUINGIA SOKONI MUDA WOWOTE.
Ray amesema kuwa filamu yake ya SISTER MARRY iliyozua kasheshe na viongozi wa kidini kutoka kanisa katoliki hivi karibuni haijazuiliwa kabisa bali ameambiwa arekebishe baadhi ya vipande katika filamu hiyo hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula filamu hiyo itaingia sokoni kila kitu kikikamilika. The film stars Vicent Kigosi(Ray), Irene Uwoya, Blandina Chagula(Johari) and Grace Mapunda.
CAG akabidhi Ripoti ya ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2011-2012 kwa Rais Kikwete.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Bwana Ludovick Utouh
akikabidhi Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2011-2012
kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.(picha
na Freddy Maro).
Subscribe to:
Posts (Atom)