Saturday, June 07, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 07, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUAGIZA MAITI IKATWE MIGUU...!!!


Mwandalizi mmoja wa mazishi nchini Afrika Kusini, anayedaiwa kuwaagiza wafanyakazi wake kuikata miguu ya maiti moja aliyodai kuwa ndefu sana alifikishwa mahakamani Ijumaa.
Ronel Mostert anayemiliki chumba cha kuhifadhi maiti ambacho pia huendesha shughuli za mazishi, alitoa amri hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa maiti hiyo ingetosha katika jeneza. Anakabiliwa na kosa la kumkata miguu maiti.
Mfanyakazi mmoja aliimbia mahakama kuwa Ronel alimuagiza kuchukua kifaa kimoja cha kukata ili kuikata miguu hiyo ya marehemu na kwamba jambo hilo limekuwa likimsumbua sana kimawazo.
Mwili marehemu ulifukuliwa ili kusaidia katika uchunguzi wa polisi.Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC

MADEREVA WA UMMA WAGOMA BRAZIL

Mgomo wa wafanyakazi hao umesababisha uhaba wa magari ya usafiri
Maafisa wa polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika siku ya pili ya mgomo wa wafanyikazi wa sekta ya uchukuzi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa usafiri wa uma katika mji wa Sao Paulo.
Takriban nusu ya vituo vya treni vilifungwa na kusababisha msongamano mkubwa wa watu katika barabara za mji huo mkubwa ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe la dunia kuanzia alhamisi ijayo.
Wafanyakazi hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi.
Awamu nyengine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo utaendelea kwa mda usiojulikana. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC

MWEGANE YEYA WA MBEYA CITY AAHIDI MAKUBWA TAIFA STARS, AMSHUKURU MUNGU KWA KUITWA NA MART NOOIJ


Mwagane-Yeya.pngnnnnnnnnnnnnnnNa Baraka Mpenja, Dar es salaam
MSHAMBULIAJI hatari wa Mbeya City fc, Mwegane Yeya amefurahishwa na kitendo cha kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij.
Akizungumza na mtandao huu, Mwegane amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kupata nafasi hiyo kwasababu Tanzania ina wachezaji wengi wenye viwango vya hali ya juu, lakini amechaguliwa yeye.
“Hii ni nafasi nyingine muhimu kwangu. Niliwahi kuitwa katika kikosi cha Young Future Taifa Stars na Kim Poulsen, lakini sikufanya vizuri kwasababu nilikuwa majeruhi. Naamini kwasasa nitaitumia vizuri nafasi hii”. Alisema Mwegane ambaye ni hatari kwa kufunga magoli ya kichwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...