Friday, January 08, 2016

WAZIRI ACHUKIZWA NA MADARAJA YA UFAULU

VITA ya kupambana na utendaji kazi usiokuwa na tija kwa Taifa kwa watendaji wengi wa taasisi za Serikali imezidi kushika kasi baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kumtaka Katibu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Charles Msonde kumwandikia maelezo ya kitaalamu yaliyosababisha kubadilishwa kwa mfumo wa upangaji viwango vya ufaulu kutoka wa madaraja (Division) hadi wastani wa pointi (GPA).

Pia amemtaka kumweleza sababu zilizowafanya kuongeza mtihani (Continuous Assesment) kwa wanafunzi wa kujitegemea ili ajiridhishe pamoja na viongozi wengine wa wizara iwapo mabadiliko hayo yana tija kwa Taifa au la.

Profesa Ndalichako alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza kwenye kikao cha menejimenti ya baraza hilo.

MKAPA AJITOSA KUMSAIDIA MAGUFULI

Rais Dk John Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu jijini Dar. Picha na Ikulu

Rais mstaafu Benjamin Mkapa amesema yuko tayari kufanya kazi yoyote na kutoa ushirikiano wake kwa serikali ya Rais John Magufuli endapo atahitajika.

Mkapa aliyeambatana na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba ametoa kauli hiyo jana punde baada ya kukutana na Rais John Magufuli Ikulu, Dar es Salaam.

“Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo,” taarifa iliyotolewa na Ikulu jana mchana imeeleza.

SAMATTA, AUBAMEYANG WATISHA TUZO ZA AFRIKA

Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mmbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika. Huku tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika ikienda kwa Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kabumbumbu katika klabu ya Borusia Dotmund nchini Ujerumani.

Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria.

Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon

YANGA YATINGA NUSU FAINALI MAPINDUZI CUP

Mabingwa wa Tanzania Bara Timu ya Yanga, imefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali kufuatia ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Mtibwa mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Aboubakar na Malimi Busungu na kuwa kinara wa kundi B la michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 7.

Katika mchezo mwingine wa mapema kutinga hatua ya nu Nusu Fainali Timu ya Mafunzo imeichapa Azam FC 2-1 kwa ushindi usio na faida kwa timu hiyo baada ya kutupwa nje ya mashindano hayo kwa uchache wa pointi.

Yanga sasa watacheza Nusu Fainali na Mshindi wa Pili wa Kundi A na Mtibwa Sugar kukutana na Mshindi wa Kundi hilo.

Kundi A linamaliza Mechi zake leo Ijumaa kwa Timu ya Jamhuri kuchuana na URA na Simba ikicheza na JKU huku kila Timu ikiwa ina nafasi kutinga Nusu Fainali ikipata matokeo mazuri ingawa Sare kwa Simba itawafikisha Nusu Fainali wakati URA na Jamhuri zikihitaji ushindi.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...