Harufu
ya rushwa! Safu ya ulinzi katika maduka ya biashara ya Mlimani City,
Dar kwenye geti la kuingilia na lile la kutokea, inadaiwa kutawaliwa na
rushwa ambapo walinzi wamenaswa ‘laivu’ wakipokea ‘mlungula’.
Kwa mujibu wa walalamikaji, walinzi hao wanadaiwa kujiwekea utaratibu usiyo rasmi chini ya kampuni ya ulinzi wa eneo hilo iliyotajwa kwa jina la Omega Nitro Risk Solutions ya jijini Dar ambapo ‘vijana’ wake wanatuhumiwa kutoza watu faini ya shilingi elfu kumi kwa gari ambalo mhusika wake amepoteza kadi ya kuingia na kutoka.
Madai hayo yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kumekuwa hakuna utaratibu mahususi kwenye ishu hiyo kwani baadhi ya walinzi kila mmoja hujiamulia kuchukua fedha bila mhusika kupewa risiti ya malipo. “Kuna tatizo kwenye safu ya ulinzi, huwa tunatozwa faini shilingi elfu kumi ukipoteza kadi,” alisema mmoja wa walalamikaji hao.