Saturday, March 15, 2014

HELKOPTA YA CHADEMA YAPIGWA MARUFUKU KUONEKANA ANGA LA KALENGA

JESHI la Polisi, limepiga marufuku chama chochote kurusha helkopta kwenye anga la jimbo la Kalenga, na limeahidi kushughulikia kikamilifu kundi au yeyote atakayejaribu kusababisha au kufanya vujo wakati wa uchaguzi na matokeo ya uchaguzi huo.
Onyo hilo limetolewa asubuhi hii na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, wakati akieleza Polisi ilivyojiandaa kuhakikisha uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, unafanyika kwa amani na utulivu, Jumapili hii, ya Marchi 16, 2014.
Kamanda Mungi amesema, Intelijensia ya jeshi hilo, imeshawabaini watu ambao wameletwa na baadhi ya vyama vinavyoshiriki kwenye uchaguzi huo, wakitokea mikoa mbalimbali kwa lengo la kufanya vurugu au kutisha wananchi wakati wa kupiga kura na kwamba ikiwa watathubutu kufanya vurugu watakiona cha moto.

“Tunafahamu na tunawajua watu walioletwa na baadhi ya vyama kwa lengo la kufanya vujo hapa Kalenga. Nawatahadharisha watu hao wajue kwamba wakijaribu kufanya vurugu, waliowaleta wataondoka halafu sisi tutabaki nao hapa Iringa kuhakikisha wanakiona cha moto”, alisema kamanda wa Polisi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

ALIYEKUWA RAIS WA SIERRA LEONE AFARIKI DUNIA

Marehemu AL Hajj Kabbah
Amefariki nyumbani kwake akiwa na miaka 82.Alhaji Ahmad Tejan Kabbah alizaliwa February 16, 1932. Aliongoza Sierra Leone kati ya mwaka wa 1996 hadi 1997 na kisha tena mwaka wa 98 hadi mwaka wa 2007.
Katika miaka mingi ya utu uzima wake, alihudumu kama mtaalamu wa uchumi na sheria. Alifanya kazi kwa miaka mingi na shirika la maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP. Baada ya kujiuzulu kutoka umoja huo mwaka wa 92, alirudi zake nchini Sierra Leone na kujiingiza katika siasa za nchi hiyo
Maisha yake ya siasaMnamo mwaka wa tisini na sita, bwana Kabbah alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama Sierra Leone's People's Party (SLPP) na kuwania urais kwa tikiti ya chama hicho mwaka wa 96.
Katika kinyanganyiro hicho, alishinda na kuwa rais kwa 59% ya kura na kumpiku mpinzani wake mkuu John Karefa-Smart wa chama cha United National People's Party (UNPP) aliyepata 40% tu ya kura.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

DUNIA IMEISHA... BABU ADAIWA KUMBAKA MJUKUU WAKE...!!!


BABU mwenye umri wa miaka (80), Benedict mkazi wa Tandika Kilimahewa, jijini Dar ametiwa mbaroni kwa madai ya kumbaka mjukuu wake wa kike (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka (6). 
Tukio hilo la kuhuzunisha linadaiwa kutokea Machi 8, mwaka huu usiku wakati babu na mjukuu wake huyo wakiwa wamelala pamoja chumbani kwake.
Akizungumza na mwandishi wetu, jirani wa babu huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alidai kwamba aliyegundua mtoto huyo kabakwa ni mjumbe wa nyumba kumi wa eneo analoishi mtuhumiwa anayefahamika kwa jina la Bibi China.
“Sisi hatukuwa na habari ila mjumbe wetu aliposikia watoto wakisema nguo ya ndani ya mwenzao (mtoto aliyebakwa) ilikuwa na damu alimwita na kumkagua, alipomuuliza alipatwa na nini akamwambia babu yake alimfanyia mchezo mbaya,” alidai jirani huyo. 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

DANIEL STURRIDGE MCHEZAJI BORA WA MWEZI ENGLAND, SAM ALLARDYCE KOCHA BORA

Daniel Sturridge akiwa na tuzo ya Mchezaji Bora wa Februari
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England kwa mwezi Februari, baada ya kufunga mabao matano katika mechi nne.
Nyota huyo ameisaidia Liverpool kushinda dhidi ya Swansea na Fulham pamoja na kuitandika mabao 5-1 Arsenal timu hiyo ya Anfield ikiweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa.
Winning: Sam Allardyce led West Ham into the top 10 with four wins from four last month
Sam Allardyce ameiongoza West Ham kuingia kwenye 10 Bora kwa kushinda mechi nne mwezi uliopita
Kocha wa West Ham, Sam Allardyce, ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi baada ya kuiongoza timu yake kushinda mechi nne. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA WAAPISHWAMJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta akila kiapo mbele ya  Katibu wa Bunge hilo Bw. Yahya Khamis Hamad, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila.
>Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akila kiapo mbele ya Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.Kulia ni Katibu wa Bunge Hilo Yahya Khamis Hamad.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MARCHI 15, 20014, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

ULI HOUNESS AJIUZULU NAFASI YA URAISI WA FC BAYERN MUNICH

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...