Tuesday, August 06, 2013

NI AIBU TANZANIA KUWA KITOVU CHA DAWA ZA KULEVYA....!!!

Dk. Harrison Mwakyembe.

KWANZA kama ilivyo ada tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuiona siku ya leo, hakika anatupenda sote na hana ubaguzi.
Baada ya kusema hayo tugeukie mada ya leo. Nchi hii miaka nenda rudi tumekuwa na sifa moja kubwa kuwa taifa lenye amani na utulivu miongoni mwa mataifa katika Bara la Afrika na duniani kwa ujumla.
Sifa hiyo sasa imegeuka na kuonekana sisi ni mabingwa wa kusafirisha dawa za kulevya. Hakika hili la kubobea katika biashara ya dawa za kulevya siyo sifa ya kujivunia hata kidogo mbele ya mataifa.

Hakuna siri wala kificho kwamba Tanzania sasa imejizolea medani za aibu kimataifa kwani katika miaka ya hivi karibuni, imekuwa na  sifa ya kuwa moja ya vinara wa biashara ya dawa za kulevya duniani.


 Ni aibu na ni sifa inayochafua taswira ya nchi yetu, kwani hivi sasa Watanzania wanaosafiri nje ya nchi wanaficha nyuso zao kwa aibu kutokana na upekuzi wa aina yake wanaofanyiwa na mamlaka za forodha na uhamiaji katika nchi wanazopitia.

TENDWA ASTAAFU, JAJI FRANCIS MUTUNGI ACHUKUA NAFASI YAKE

8 39276

Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alipata kusema; “ Tatizo kubwa kwa nchi za Afrika si nakisi kwenye bajeti zao, bali, nakisi ya IMANI”.
Na Profesa Gaudence Mpangala naye amepata kusema; “ Msingi wa matatizo yetu mengi ni uwepo wa mfumo wa Chama Dola.”

Na kwangu mimi, changamoto kubwa kwa Katiba yetu ijayo ni kuona kama itatoa nafuu ya hayo mawili hapo juu.

Maana, haiyumkini tukafanikiwa kujenga taifa la kisasa kama
tutakosa ujasiri wa kuzipa  mgongo  kanuni na taratibu za kijima kwa maana ya taratibu  za kizamani.

Jakaya Kikwete ameonyesha kuwa mfano wa kiongozi mwenye ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni na taratibu za kijima. Swali, ni wangapi wengine kwenye mfumo anaoutumikia wenye mitazamo kama ya kwake? Maana, maamuzi mengine ya kimageuzi anayoyafanya Kikwete yasingeweza kufikiriwa miaka kumi iliyopita.

Jana Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa Jaji  Francis Mutungi  kushika nafasi ya John Tendwa kama Msajili wa Vyama. Ukweli unabaki, kuwa kwenye utendaji wake, Tendwa kama mlezi hakuaminika na baadhi ya aliowalea. Hilo ni pungufu kubwa na linakwaza juhudi za kukuza demokrasia ya nchi. Msajili wa vyama vya siasa anapaswa aonekane kuwa ni  mlezi wa vyama vya siasa na wala si mwonezi wa vyama vya siasa. Na kazi ya ulezi inatakiwa ionekane.


AJALI MBAYA YATOKEA MSWISWI MKOANI MBEYA MMOJA AFARIKI PAPO HAPO...!!!

GARI AINA YA TOYOTA COROLLA  ILIYOGONGANA NA BASI LA HOOD MENEO YA MSWISWI MBEYA DEREVA WA GARI NDOGO AMEFARIKI PAPO HAPO

HATI YA KUSAFIRIA YA MAREHEMU DAVIS HANAMUNDE MZAMBIA

MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 06, 2013

DSC 6297 a9f0b
DSC 6298 c66d3

MGOMBEA ALITUMIA ZIWA NYASA KUJIPIGIA DEBE MALAWI

banda e1188

Mgombea Urais wa Democratic Progressive Party (DPP) nchini Malawi, Peter Mutharika, amesema hakuna sababu za kufanya majadiliano kuhusu Ziwa Malawi ambalo Tanzania wanaliita Ziwa Nyasa. (HM)


Mutharika, ambaye ni mwanasheria, aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi  Mkoa wa Kati.

Akikaririwa na gazeti la  Nyasa Times, Mutharika  alisema Tanzania haina cha kuambulia kwa Ziwa Malawi.

Kiongozi huyo ambaye hakuwapo katika mkutano wa Rais Joyce Banda na wapinzani kuzungumzia mustakabali wa ziwa, aliwahakikishia Wamalawi kuwa wasiwe na wasiwasi wa mvutano huo.

TAARIFA YA SIKU KUU YA EID KUTOKA JESHI LA POLISI


3 c9818
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA



Anuani ya Simu “ MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                   Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                                    Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                         S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                                    DAR ES SALAAM.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar Es Salaam Agosti 06, 2013.

Ndugu Wanahabari,


Jeshi la Polisi Nchini linatoa shukrani kwa wananchi wote wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa dini, wanasiasa, makampuni binafsi ya ulinzi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa njia mbalimbali katika kuhakikisha kwamba nchi yetu ya Tanzania inakuwa salama na raia wote wanaishi kwa amani na utulivu bila hofu ya uhalifu na wahalifu.


Katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki na za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo wanamoishi na sehemu mbalimbali zikiwemo maeneo ya biashara.


Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu. Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu, pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...