Wednesday, September 10, 2014

KIKWETE AWATIMUA MAKADA WA CCM WALIOKUSANYIKA KUMPOKEA...!!!

Rais Jakaya Kikwete jana aliwafukuza makada wa CCM waliokuwa wakimsubiri kwenye kituo cha dharura cha ebola alipokitembelea kwa kushtukiza katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Makada hao ambao baadhi yao walivalia sare za CCM, kinyume na matarajio yao, kiongozi huyo alipofika hospitalini hapo alionyesha kuwashangaa kabla ya kuwataka waondoke kwa kuwa hakuhitaji kuzungumza nao, bali wasimamizi wa kituo hicho.
“Hawa watu wote wanafanya nini hapa! Sijaja kuhutubia hapa mimi. Ndugu zangu hawa waliowaita wamewasumbua bure, nawashukuruni sana kwa kuja, endeleeni na shughuli zenu,” alisema Rais Kikwete ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki.
Hatua hiyo ilionekana kuwanyong’onyeza makada hao ambao hawakuwa na jinsi isipokuwa kuondoka taratibu kwenye eneo hilo na kumwacha Rais Kikwete na viongozi wa kituo hicho.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ZITTO "SIWEZI KUJIUNGA NA UKAWA"

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe. PICHA|MAKTABA 

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hawezi kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa sababu baadhi ya wajumbe wa umoja huo hawautaki Muungano na wamejificha nyuma ya pazia la kutaka muundo wa serikali tatu.
Amesema si kila mtu anayetaka serikali tatu anaupenda Muungano na kusisitiza kuwa ni aibu kuwa na marais watatu ndani ya nchi moja.
“Msimamo wangu wa serikali tatu si msimamo wa marais watatu kwa sababu najua msimamo wa marais watatu utavunja nchi. Msimamo wangu ni rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano, Mkuu wa Serikali Zanzibar na Mkuu wa Serikali Bara,” alisema.
Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya Chadema, moja ya vyama vinavyounda Ukawa, alitoa ufafanuzi huo wiki iliyopita katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 10, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MTOTO WA OBASANJO APIGWA RISASI NIGERIA

Wanamgambo wa Boko Haram
Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na wanamgambo wa kiislamu Boko Haram.
Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa siku ya jumatatu wakati jeshi la Nigeria lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa Michika karibu na mji wa Mubi mji uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa.
Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo ameiambia BBC kuwa kanali Adeboye anaendela vizuri.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao, wanajeshi wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo katika jimbo hilo kufungwa.
Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji mingi kaskazini mashariki na kutangaza kuwa himaya za kiislamu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

MLIPUKO WAUA VIONGOZI WA WAASI SYRIA

Waasi wakipambana nchini Syria
Wanachama 50 wa kundi moja la waasi wa Syria wameuawa au kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga.
Vyombo vya habari vya serikali na wanaharakati wanasema mshambuliaji wa kujilipua aliilenga nyumba moja katika jimbo la Idlib, ambamo viongozi wa Ahrar al-Sham walikuwa wakikutana.
Kamanda wa kikundi hicho Hassan Abboud ni miongoni mwa watu waliouawa.
Kiongozi huyo ameuawa pamoja na makamanda wengine wa ngazi za juu wa kikundi hicho. Shambulio hilo limefanywa na mtu aliyejilipua katika mji wa Ram Hamdan kaskazini magharibi mwa Syria.
Ahrar al Sham ni sehemu ya kikundi cha Islamic State, muungano wa vikundi saba vya waasi wa kiislamu nchini Syria. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

YANGA HIYOOOO MPAKA FIFA

Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.

Uongozi wa Yanga umepanga kuliandikia Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) kuishtaki TFF kwa kukiuka Kanuni ya 19 ya usajili katika kufanya uamuzi wa utata wa usajili wa mshambuliaji wa Uganda, Emmanuel Okwi.
Kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kilichofanyika jijini Dar es salaam juzi, kiliamua kumtangaza Okwi kuwa mchezaji huru baada ya kubaini kuwa Yanga ilivunja mkataba kwa kutomlipa stahiki zake za usajili na pia kuandika barua TFF kutaka mkataba wake na Mganda huyo uvunjwe, uamuzi ambao umeinufaisha Simba ambayo imemsajili.
Mkataba wa mchezaji huyo ulipitiwa na kamati hiyo ikiwamo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na Yanga na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.
Kamati hiyo ilisema ukiwa ni mkataba wa pande mbili, Yanga ilikiuka kipengele namba nane kuhusu malipo ya ada ya usajili. Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho hadi kufikia Juni 27 mwaka huu, ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.
Hata hivyo, uongozi wa Yanga jana ulisema haukubaliani na uamuzi huo na kwamba walikuwa wameshaandika barua kupinga baadhi ya wajumbe katika kamati ya sheria ya TFF wasisikilize kesi yao, akiwamo mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ya sheria.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...