Monday, December 09, 2013

JE, UNAJUA KUWA WOGA, AIBU HUPUNGUZA KUJIAMINI KATIKA MAPENZI...??!

https://www.facebook.com/jambotz

KARIBU mpendwa wa blog yetu ya Jambo Tz inayopendwa na wengi na kuwashukuru wote wanaotumia muda wao kutupongeza wengine kutukosoa ili kuiboresha blog yetu.


Vilevile wapo walio na matatizo wanaoomba msaada ambao nashukuru umewasaidia wengi. Kama ilivyo ada, umekaa mkao wa kula kutaka kujua leo nimekuja na mpya gani. Nasema hakuna jipya chini ya jua kwa sababu kitu mapenzi kilikuwapo tangu enzi ya mababu na hata hao waliyakuta tokea enzi ya Adamu na Eva.
Tumepata malalamiko mengi kutoka kwa wasomaji wetu waliolalamika juu ya matatizo wanayokumbana nayo katika kula chakula cha roho, wengi wanalalamika kuwa hawali chakula kilichokamilika.
Kwa mfano mtu anauliza; Mbona mpenzi wangu si mtaalam wa mambo flani?, wengine hudiriki kusema tangu waanze mapenzi na waume zao au wake zao hawajafurahia mapenzi na kushangaa kusikia mapenzi yakikukolea hukufanya upandishe mashetani na kumaliza maneno yote mdomoni au kumfanya mwanaume atoe ahadi ambazo hana hata uwezo nazo kwa kusema atakununulia ndege wakati hata baiskeli hana.

Yote hayo ni mtu kuguswa pale panapomfanya ajione yupo dunia nyingine na kujiona juu hayupo wala chini hayupo. Wao hujiuliza kulikoni wenzao wafaidi wao wasifaidi kwani wamekosa nini.

Swadakta swali zuri sana, kumekuwa na utamaduni wa watu wengi kuona aibu kuuliza jambo walisilolijua hasa katika mapenzi hii imepelekea watu kuwa wavivu kujifunza kwa kuona aibu kuuliza kitu wasichokijua kwa kuogopa kuitwa washamba.
Nani alikuambia wote wamezaliwa wanajua, usichokijua uliza usisubiri aibu ikukute kwa mpenzio, kuuliza nje au kutoa nje udhaifu wako. Siku zote wasiojua huwa wajanja sana ili kuficha udhaifu wao lakini unauficha udhaifu wako wakati lazima uingie kwenye gemu.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU YA MIAKA 52 YA UHURU DESEMBA 09, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.

MARAIS KUINGIA KWA KADI MAZISHI YA MANDELA...!!!



Qunu, nyumbani kwa Mandela 
TISHIO la vitendo vya kigaidi vinavyotokea kwenye maeneo mbalimbali hapa duniani, vimeifanya Serikali ya Afrika Kusini, kutoa kadi kwa marais na viongozi watakaohudhuria mazishi ya baba wa taifa hilo, Nelson Mandela. Mandela aliyefariki Desemba 5, atazikwa Desemba 15 kijijini kwake Qunu, eneo alilolichagua kabla ya mauti yake. 
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya kimataifa, usalama katika miji ya Afrika Kusini, unatarajiwa kuimarishwa zaidi kuliko hata ule unaotumika kwa marais wa Marekani wanapofanya ziara kwenye mataifa mbalimbali.  
Taarifa hizo zinabainisha kutokana na idadi kubwa ya watu kuhudhuria mazishi hayo, utawala wa nchi hiyo umebuni mbinu hiyo ya utoaji kadi kwa watu watakaokuwa eneo la maziko wakiamini itasaidia kuimarisha ulinzi.  
Mazishi hayo yanatarajiwa kuvunja rekodi ambapo yanalinganishwa na yale ya Papa John Paul II mwaka 2005, ambayo yalihudhuriwa na wafalme watano, malkia sita wa falme mbalimbali na marais wapatao 70 na mawaziri kadhaa, wakiwamo wafuasi wake zaidi ya milioni mbili.  
Ratiba ya kutoa heshma za mwisho yatangazwa Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na Serikali ya Afrika Kusini, mwili wa Mandela utawekwa katika jengo la serikali kwa muda wa siku tatu, kutoa fursa kwa wananchi kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi waliyempenda. Meya wa jiji la Cape Town, Patricia de Lille, alisema ibada ya kumuaga Mandela itafanyika Jumanne kwenye uwanja wa mpira mjini Johannesburg.  
Jana maelfu ya raia wa Afrika kusini kutoka matabaka yote na rika zote walishiriki katika ibada ya pamoja ya dini mbalimbali, ambayo ilifanyika mjini Cape Town mahali ambako Mandela alitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuachiwa huru kutoka jela. 
Chanzo: TANZANIA DAIMA

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...