Monday, May 19, 2014

VAN GAAL AMTEUA VAN PERSIE KUWA NAHODHA MPYA MAN UNITED

Double Dutch: Louis van Gaal (right) sees Robin van Persie as his perfect captain at Manchester United
 Waholanzi wawili: Louis van Gaal (kulia) anaona Robin van Persie ndiye nahodha aliyekamilika katika klabu ya Manchester United.
LOUIS van Gaal  anatarajia kumteua mshambuliaji wake hatari Robin van Persie kuwa nahodha wa kikosi chake mara atakapojiunga na Manchester United baada ya kumalizika kwa kombe la dunia majira ya kiangazi nchini Brazil.
Jumamosi iliyopita Van Persia aliifungia bao muhimu timu ya taifa ya Uholanzi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador na kulazmisha sare ya 1-1.
Van Gaal amekuwa na mahusiano mazuri na RVP ambaye ni nahodha wa timu ya taifa na sasa anatarajia kumpa jukumu hilo katika klabu ya Man United na kumpiga chini Rooney ambaye angekuwa nahodha wa kudumu katika utawala wa David Moyes.
A sign of things to come? Van Persie (right) poses with Kluivert (left), Louis van Gaal's assistant manager
Class: Holland captain van Persie scored a fantastic volley in their 1-1 draw with Ecuador on Saturday

SAKATA LA IPTL LAZIDI KUWAVURUGA WABUNGE


KABWE_b5fd6.jpg
Dodoma. Sakata la fedha za IPTL limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wabunge kudai kurubuniwa na wenzao kwa fedha ili wakwamishe Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, wakidai balozi mmoja yuko nyuma ya mpango huo.
Katika sakata hilo, Sh200 bilioni zilizohifadhiwa kwenye akaunti ya Escrow zilitolewa na kulipwa kwa Kampuni ya Pan African Power (PAP), ambazo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amesema anachunguza akishirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru).
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto ameonya kuwa kuwaingiza mabalozi katika sakata la ufisadi wa zaidi ya Sh200 bilioni za IPTL ni kuibua mgogoro wa kidiplomasia na nchi husika.
Akizungumza na gazeti hili jana, mbunge huyo alisema kuwa kiongozi yeyote atakayegundulika kufaidika na hongo hiyo, kamati yake itaweka wazi jina lake na hakuna atakayeachwa bila kuchukuliwa hatua za kisheria.
Zitto alitoa kauli hiyo jana baada ya kubainika ujumbe mfupi wa maandishi (sms) unaodaiwa kusambazwa, ukifichua kile kinachodaiwa ni kuhongwa kwa baadhi ya wabunge ili wakwamishe bajeti ya wizara hiyo.
Ujumbe huo unasomeka: "Spika wa Bunge la Jamhuri, sisi wabunge waadilifu tunakiri kwamba Mhe. Mkono ametufuata na kutupatia fedha kila mmoja milioni 3 ili tukwamishe bajeti ya Nishati na Madini.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

COSMAS CHEKA ATAMBA KUTETEA UBINGWA WAKE WA TPBO

IMG_8710Cosmas Cheka ‘kulia’
Na Mwandishi Wetu BONDIA Cosmas Cheka anatarajia kupanda ulingoni juni mosi kwa ajili ya kutetea taji lake la ubingwa wa TPBO anaoshikilia kwa kupambana na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana social hall wa Morogoro
Akizungumzia mpambano huo Cheka amesema amejiandaa kupigana kwa raundi kumi hivyo mashabiki waje kuona kazi anayoifanya akiwa ulingoni. Bondia huyo ambaye anatamba sambamba na kaka yake Fransic Cheka aliyekuwa bingwa wa WBF ambao alivuliwa kizembe amesema yeye anataka afike mbali zaidi ya kaka yake huyo.
Pambano hilo linalosimamiwa na TPBO litasindikizwa na mapambano ya utangulizi kati ya Kudura Tamimu atakaeevaana na Sadiki Yusufu, wakati Mohamed Matimbwa ataoneshana umwamba na Twaha Kassimu
Siku hiyo pia kutakuwa na uuzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Mohamed Matumla vs Fransic, Miyeyusho, Japhert Kaseba Vs Thomas Mashali , Floyd Mayweathar, Manny Paquaio, Saul ‘canelo’ alverez , Mike Tyson, Mohamed Ali, Ferex Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kutakuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa zawadi kwa mabondia na Kocha Super D ambaye ameahidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta, Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakaoonesha uwezo wa hali ya juu wa kutupiana masumbwi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 19, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

'NAPE ALAANIWE KWA KUTUITA BOKO HARAM'


Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya CUF, Amina Abdallah Amour amemjia juu katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuufananisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kundi la Boko Haramu na kutaka alaaniwe.
Ukawa iliundwa wakati wa Bunge Maalumu la Katiba na unahusisha wajumbe kutoka vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF.
Akizungumza bungeni mjini Dodoma juzi, mbunge huyo alisema kauli ya Nnauye ni ya uchochezi na inapaswa kulaaniwa.
Mbunge huyo alikuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kwa mwaka 2014/2015 iliyowasilishwa na waziri wake, Sophia Simba.
“Gazeti la Uhuru (jana) lilimnukuu Nape Nnauye akisema Ukawa ni sawa na Boko Haramu… Hii ni kauli chafu na ya uchochezi. Haikubaliki na ninailaani kwa nguvu zangu zote,” alisema.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

ASKOFU "HOFU YA MUNGU ITATUPA KATIBA MPYA"


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu akiongoza watu mbalimbali kumpongeza Askofu Mkuu mpya wa Jimbo la Songea, Damian Dallu katika Kanisa la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba mjini Songea jana. Picha na Joyce Joliga 


Kwa ufupi
Hayo aliyasema jana katika Ibada maalumu ya kumsimika rasmi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Mathias Mulumba lililopo Mjini Songea ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya waumini, viongozi wa chama na Serikali, viongozi wa madhehebu ya dini pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda.

Songea. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Damian Dallu amesema Katiba Mpya itapatikana iwapo wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa na maadili ya kiroho kwa kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu bila kupindisha ukweli wa mchakato wa maoni ya Katiba.

Amesema kupotosha ukweli wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba unaweza kuipeleka nchi kubaya.

Hayo aliyasema jana katika Ibada maalumu ya kumsimika rasmi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Mathias Mulumba lililopo Mjini Songea ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya waumini, viongozi wa chama na Serikali, viongozi wa madhehebu ya dini pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WATU 6 WAUAWA KATIKA MLIPUKO NIGERIA

Mlipuko wa bomu Nigeria
Bomu lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 6 na kuwajeruhi wengine wengi.
Shambulio hilo limefanywa katika eneo linaloaminiwa kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao wamekuwa wakilengwa mara nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.
Mwandishi wa BBC mjini Abuja Will Ross anasema kuwa eneo hilo lililolengwa linajulikana kama Sabon Gari. Watu wengi walikuwa kwenye migahawa ya vileo na kwenye barabara. Amesema kuwa kilichosalia kwenye gari lililokuwa na bomu hiyo ni injini pekee.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja mji wa Kano umepumzika kutokana na mashambulio, hasa kwasababu ya oparesheni kali iliyofanywa na maafisa wa usalama kuwasaka wanamgambo hao wa Boko Haram.
'Mashambulio ya awali'
Rais Goodluck Jonathan alilazimika kufutilia mbali ziara yake mjini Chibok wiki jana kutokana na utovu wa usalama
Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.
Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

TAHADHARI USALAMA WAKO UKIWA KENYA

Kenya imekabiliwa na mashambulio kadhaa hivi karibuni
Tahadhari zaidi zimetolewa nchini Kenya za kutokea mashambulio katika baadhi ya maeneo ya umma na foleni za barabarani.
Mitandao ya kijamii ya twitter na face book imetumiwa kusambaza ujumbe miongoni mwa wananchi kutoa tahadhari hiyo.
Usalama umeimarishwa katika Ubalozi wa Marekani Kenya na ofisi za Umoja wa mataifa Nairobi, na hatua madhubuti zimechukuliwa kupunguza msongamano wa watu katika maeneo hayo.
Na huku hayo yakiarifiwa sekta ya utalii nchini humo imeendelea kupata hasara kubwa kutokana na kuondolewa kwa raia wa kigeni hasa Uingereza waliokuwa katika mji wa kitalii wa Mombasa kufuatia tishio la kulengwa katika shambulio.
Afisa Mkuu wa Shirika la kampuni linaloshughulikia utalii nchini, Kenya Tourism Federation, Agatha Juma anasema upungufu wa watalii nchini Kenya utasababisha ukosefu wa ajira, zaidi kwa raia wa Kenya wanaofanya katika hoteli mbali mbali nchini.
Kenya imeshuhudia mashambulio kadhaa katika siku za hivi karibuni katika maeneo mbali mbali nchini ukiwemo mji wa Mombasa na Nairobi, yaliosababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa.Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...