Monday, May 19, 2014

SAKATA LA IPTL LAZIDI KUWAVURUGA WABUNGE


KABWE_b5fd6.jpg
Dodoma. Sakata la fedha za IPTL limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wabunge kudai kurubuniwa na wenzao kwa fedha ili wakwamishe Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, wakidai balozi mmoja yuko nyuma ya mpango huo.
Katika sakata hilo, Sh200 bilioni zilizohifadhiwa kwenye akaunti ya Escrow zilitolewa na kulipwa kwa Kampuni ya Pan African Power (PAP), ambazo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amesema anachunguza akishirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru).
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto ameonya kuwa kuwaingiza mabalozi katika sakata la ufisadi wa zaidi ya Sh200 bilioni za IPTL ni kuibua mgogoro wa kidiplomasia na nchi husika.
Akizungumza na gazeti hili jana, mbunge huyo alisema kuwa kiongozi yeyote atakayegundulika kufaidika na hongo hiyo, kamati yake itaweka wazi jina lake na hakuna atakayeachwa bila kuchukuliwa hatua za kisheria.
Zitto alitoa kauli hiyo jana baada ya kubainika ujumbe mfupi wa maandishi (sms) unaodaiwa kusambazwa, ukifichua kile kinachodaiwa ni kuhongwa kwa baadhi ya wabunge ili wakwamishe bajeti ya wizara hiyo.
Ujumbe huo unasomeka: "Spika wa Bunge la Jamhuri, sisi wabunge waadilifu tunakiri kwamba Mhe. Mkono ametufuata na kutupatia fedha kila mmoja milioni 3 ili tukwamishe bajeti ya Nishati na Madini.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz


Mkono alikaririwa na Mwananchi Jumapili akikiri kufahamu kuhusu ujumbe huo na kuwa amelalamika kwa Spika juu ya jambo hilo. "Ni kweli nimelalamika kwa Spika. Unajua utaratibu wa Bunge ni kuwa kama kuna malalamiko unaliwasilisha rasmi kwa Spika.. hilo jambo lipo nimelifikisha kwa Spika na wao ndio watafuatilia kwa utaratibu wao," alisema.
Zitto alisema hatarajii mbunge yeyote kutumia suala la IPTL kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwani uchunguzi juu ya sakata hilo bado unafanywa na vyombo vya kiuchunguzi.
"Ninatia shaka ni kwa nini viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini waweweseke wakati uchunguzi bado haujakamilika. Nawasihi watu wote, wabunge na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini wasubiri uchunguzi," alisisitiza Zitto.
"CAG na Takukuru waachwe wamalize uchunguzi wao. Uchunguzi utakuja PAC na tutauweka wazi," alisema Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Zitto alisema mtu yeyote anayesambaza ujumbe huo ambao unahusisha mabalozi au balozi wa nchi yeyote, analiingiza Taifa katika mgogoro wa kidipomasia na kuwasihi wabunge wanaofanya hivyo kuacha. "Suala hili la IPTL si jambo la kwenda kuzuia bajeti ya Wizara. Bajeti ya Wizara ijadiliwe kulingana na mantiki yake, miradi ya umeme vijijini, miradi ya kuongeza uzalishaji umeme, kuondoa mgawo na kupunguza gharama za umeme," alisema.
"CAG na Takukuru wanalifanyia kazi suala la IPTL, sasa lisifanywe siasa. Hakuna mtu yeyote ambaye amefaidika na ufisadi huo ambaye ataachwa bila kuchukuliwa hatua zinazostahili," alisisitiza Zitto
Hali kadhalika alimtaka mtu yeyote mwenye taarifa za kuhongwa ili kuzuia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kupeleka taarifa hiyo kwa Spika na kuacha kuzusha uvumi wa kuhongwa wabunge kila inapokaribia bajeti ya wizara hiyo.
Sakata la IPTL liliibuliwa bungeni wiki iliyopita na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye alisema kuna ufisadi wa zaidi ya Sh200 bilioni katika akaunti ya Escrow iliyopo chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...