Waholanzi
wawili: Louis van Gaal (kulia) anaona Robin van Persie ndiye nahodha
aliyekamilika katika klabu ya Manchester United.
LOUIS
van Gaal anatarajia kumteua mshambuliaji wake hatari Robin van Persie
kuwa nahodha wa kikosi chake mara atakapojiunga na Manchester United
baada ya kumalizika kwa kombe la dunia majira ya kiangazi nchini Brazil.
Jumamosi
iliyopita Van Persia aliifungia bao muhimu timu ya taifa ya Uholanzi
katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador na kulazmisha sare ya 1-1.
Van
Gaal amekuwa na mahusiano mazuri na RVP ambaye ni nahodha wa timu ya
taifa na sasa anatarajia kumpa jukumu hilo katika klabu ya Man United na
kumpiga chini Rooney ambaye angekuwa nahodha wa kudumu katika utawala
wa David Moyes.
Van Persie alikuwa na majeruhi kwa muda wa wiki sita za mwishoni mwa
msimu mbovu wa Man United baada ya kuumia goti katika mechi ya UEFA
dhidi ya Olympiacos mwezi machi mwaka huu.
‘Hata
kama ametokea katika majeruhi, alifunga bao la maajabu, bao ambalo
huwezi kuamini, ni bao zuri mno,’ alisema Van Gaal baada ya
mshambuliaji huyo kusawazisha dakika ya 37 katika uwanja wa Amsterdam
ArenA jumamosi.
Kwa
mujibu wa Van Gaal, kwa asimilia 100, Van Persie hayuko fiti lakini
alionekana kuwa imara na kuitendea haki pasi ya Feyenoord na kufunga bao
muhimu.
‘Nilifurahishwa
na kiwango chake, pia ni nahodha wa aina yake,” Alisema Van Gaal.
“Nadhani unampa mchezaji unahodha kama mna morali na falsafa
inayofanana”.
“Sio tu mambo ya uwanjani na kiwango cha mchezaji, hata maisha ya kawaida tu”.
“Naamini
hilo ni muhimu sana. Naamini Van Persie na Van Gaal tuna falsafa moja”.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment