Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya
CUF, Amina Abdallah Amour amemjia juu katibu wa itikadi na uenezi wa
CCM, Nape Nnauye kwa kuufananisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na
kundi la Boko Haramu na kutaka alaaniwe.
Ukawa iliundwa wakati wa Bunge Maalumu la Katiba na unahusisha wajumbe kutoka vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF.
Akizungumza bungeni mjini Dodoma juzi, mbunge huyo alisema kauli ya Nnauye ni ya uchochezi na inapaswa kulaaniwa.
Mbunge huyo alikuwa akichangia hotuba ya makadirio
ya mapato na matumizi ya Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kwa mwaka
2014/2015 iliyowasilishwa na waziri wake, Sophia Simba.
“Gazeti la Uhuru (jana) lilimnukuu Nape Nnauye
akisema Ukawa ni sawa na Boko Haramu… Hii ni kauli chafu na ya
uchochezi. Haikubaliki na ninailaani kwa nguvu zangu zote,” alisema.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Mbunge huyo alihoji “wazazi wao hawajui watoto wao
wanaishije, wanakula nini wala wanalala vipi…. Leo hii Nape Nnauye
amethubutu kusema Ukawa ni sawa na Boko Haramu?”
Hata hivyo, wakati akihoji hivyo, baadhi ya Wabunge wa CCM nao walisikika wakihoji “na Intarahamwe Je?”.
Ukawa ilitumia jina hilo la Interahamwe wakati
mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akitangaza uamuzi wa kundi
hilo kujitoa kwenye Bunge la Katiba, akiifananisha CCM na kundi hilo la
nchini Rwanda.
Katika gazeti hilo, Nnauye amenukuliwa akisema
Ukawa ni kundi hatari linaloeneza chuki na kusambaza uongo kwa Wananchi
kwa nia ya kuwagawa na kusema silaha wanazotumia ni zaidi ya Boko
Haramu.
Nnauye anadaiwa kutoa kauli hiyo katika mkutano wa
hadhara uliofanyika mkoani Tabora, akisema silaha za uongo wanazotumia
viongozi wa Ukawa ni hatari zaidi kuliko silaha za moto zinazotumiwa na
Boko Haramu.
Viongozi wa CCM na wale wa Ukawa wamekuwa
wakizunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kufafanua kile
kilichojitokeza ndani ya Bunge la Katiba na kusababisha Ukawa kususia
Bunge hilo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment