Monday, March 16, 2015

WAHAMIAJI 64 KUTOKA ETHIOPIA WAKAMATWA

Ramani ya Tanzania
Polisi mkoa wa Dodoma nchini Tanzania wanawashikilia wahamiaji haram 64 raia wa Ethiopia, huku mmoja wao akipatikana akiwa amekufa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amenukuliwa akisema wanamshikilia dereva wa gari lililokuwa limewabeba watu hao ambao inaaminika walikuwa njiani kuelekea kusini mwa Afrika.
Hii si mara ya kwanza kwa wahamiaji wa aina hiyo kukamatwa katika mazingira hayo.
Mwaka 2012 watu 42 kutoka Eritrea walikutwa wamekufa katika lori mkoa wa Dodoma kwa kile kinachosemekana ni kukosa hewa kutokana na kufichwa ndani ya lori hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAMILIONI WAANDAMANA BRAZIL

Rais Dilma Roussef wa Brazil
Zaidi ya watu milioni moja kutoka nchini Brazil wameandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff, huku wengi wao wakitaka rais huyo afunguliwe mashtaka ya ufisadi mkubwa uliofanyika katika shirika la mafuta la serikali, Petrobras.
Maandamano kama hayo yamefanyika katika miji mingi ya Brazil ikiwemo mji mkuu wa nchi hiyo Brasilia.
Maandamano makubwa kabisa yamefanyika katika mji wa Sao Paulo ambalo ni eneo la upinzani waliokuwa wakipita mitaani.
Mmoja wa waandamanaji Francisco Pestana alilalama akisema"Dilma hana uwezo wa kuongoza nchi yetu. Tunachokabiliwa nacho ni bahati mbaya sana, namna mamabo yanavyokwenda, yanaweza kuelekea kubaya zaidi, tutakuwa Venezuela nyingine."
Naye mwandamanaji mwingine mwanamke Janaina Lima anasema "leo ni maandamano ya watu. Watu wamejitokeza mtaani kusema hakuna ghasia zaidi, hakuna rushwa, hakuna uvivu zaidi, hakuna uzembe zaidi, hakuna utawala mbaya. Na kuunga mkono Brazil mpya." Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC

YANGA YAIADHIBU PLATNUM YA ZIMBABWE 5-1

Kikosi cha Yanga kilichoisambaratisha Platnum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1
Timu pekee iliyobakia kwenye mashindano ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika kutoka Tanzania, Yanga, imeendelea kuweka matumaini hai ya kusonga mbele baada ya kuiangushia kipigo kikali timu ya Platnum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1.
Mchezo huo wa raundi ya kwanza ya vilabu vinavyoshiriki Kombe la Shirikisho la CAF, ulifanyika Jumapili jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa kufungana mabao 2-1.
Kipindi cha Pili ndicho kilichokuwa kiama chya Platnum baada ya kuruhusu mabao matatu zaidi.
Wafungaji wa timu ya Yanga ni Mrisho Ngasa aliyefunga magoli mawili, Haruna Niyonzima, Salum Telela, na Amisi Tambwe walifunga bao moja kila mmoja. Kwa matokeo hayo Yanga imejenga mazingira ya kusonga mbele. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...