Friday, October 17, 2014

CHADEMA WAANZA SAFARI YA KUPINGA KATIBA NCHI NZIMA

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akizungumza kwenye mkutano na waandishi Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Issa Mohamed. 

Kamati Kuu ya Chadema imeazimia kuendesha kampeni ya kupinga Katiba Inayopendekezwa kwa viongozi wake wakuu pamoja na wale wa mabaraza yake kufanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini.
Hatua hiyo imekuja siku tatu, tangu Rais Kikwete autangazie umma wa Watanzania alipokuwa akihutubia kilele cha Mbio za Mwenge mkoani Tabora kwamba Katiba Inayopendekezwa inafaa hivyo kuwataka Watanzania waipigie kura wakati wa mchakato wa kura ya maoni.
Ziara ya Chadema itaanzia katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambako itachukua siku 20 ikiongozwa na Baraza la Wanawake (Bawacha), linaloongozwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na baada ya kumaliza, itaanza ziara nyingine ya siku 20 itakayofanywa na Baraza la Vijana (Bavicha).
Dk Slaa alisema CCM wameanza kazi ya kuwataka wananchi kupiga kura ya ‘ndiyo’ na Chadema wanaanza mikutano ya kuwashawishi wananchi kuikataa kwa kuipigia kura ya ‘hapana’.
Alisema kuanzia Novemba 5 mwaka huu, viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho nao wataanza ziara katika mikoa mbalimbali nchini.
“Bawacha ndiyo itakuwa timu ya kwanza. Itakwenda Mwanza mjini, Ukerewe, Magu, Sengerema, Geita, Busanda, Bukombe, Biharamulo, Muleba, Karagwe, Bukoba Mjini, Chato, Shinyanga Mjini na Maswa Mashariki,” alisema Dk Slaa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WARIOBA: MSIKURUPUKE KUPITISHA KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. Picha na Maktaba 

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka Watanzania kutokurupuka kuipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa kuwa imeyaacha kando maoni yao mengi na akawataka waisome kwa makini kabla ya kuikubali au kuikataa.
Akiwa katika likizo ya wiki moja nyumbani kwake Bunda, Mkoa wa Mara, Jaji Warioba alialikwa na vijana wa mji huo kupitia Jukwaa lao la Uwazi na Fikra Yakinifu, wakiomba azungumze nao kuhusu masuala mbalimbali hasa mchakato wa Katiba Mpya.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Harrieth, Jaji Warioba aliulizwa na kujibu maswali; anaionaje Katiba Inayopendekezwa na iwapo CCM imemgeuka kwa nini asihame chama?
Akijibu maswali hayo, Jaji Warioba alisema Katiba hiyo haina maoni yote ya wananchi kama Bunge Maalumu lilivyojinadi, bali yamewekwa machache ambayo hata hivyo yamo hata katika Katiba ya sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DIDA, JAJA, WABEBA JUKUMU ZITO YANGA


kipa Deogratius Munishi 'Dida' 

Pambano la watani wa jadi, Yanga na Simba kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam litakuwa mtihani mkubwa kwa nyota watatu wa Yanga kwa sababu tofauti.

Watatu hao ni mshambuliaji, Genilson Santos ‘Jaja’ , kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na kiungo Andrey Coutinho.

Jaja, aliyeibuka shujaa ghafla alipoitungua Azam kwa mabao mawili kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, kisha akapoteza makali tangu Ligi Kuu ianze,  ana deni kubwa kwa mashabiki wenye matumaini kwake kuwa atafungua akaunti ya mabao dhidi ya Simba.

Makali yake ya Septemba 14 alipoisulubu Azam yaliyomkatia tiketi ya kuwa kipenzi cha mashabiki na  yanaweza kuongezeka au kufutika.

Mbrazili huyo kipenzi cha mashabiki wa Yanga, ingawa pia anaweza kuwa na wakati mgumu kesho kuthibitisha uwezo wake, kutetea nafasi yake kwenye kikosi  cha kwanza, akishindwa kuisaidia Yanga kuchomoza na ushindi, itakuwa tiketi yake ya kusahaulika. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 17, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

DSC04323
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...