Saturday, May 27, 2017
MAMBO YANAYOPENDEZA KATIKA MWEZI WA RAMADHANI
Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) alipanga kuwa mwaka uwe na miezi kumi na mbili, na katika hiyo akaichagua baadhi akaitukuza na kuifadhilisha zaidi ya mengine.
Mwenyezi Mungu anasema;
“Hakika idadi ya miezi mbele ya Allah ni miezi kumi na mbili kati ya hiyo mna mine iliyo mitukufu."
Nayo ni (Dhulqaada, Dhulhijja, Muharram, na Rajab).
Baada Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) kuifadhilisha miezi hii minne akaufadhilisha vile vile zaidi kuliko hata miezi hii minne mwezi tuliyo ndani yake nao ni mwezi wa Ramadhani, usiku wa cheo (Laylatul Qadr), katika mwezi huu, tokeo kubwa ni kuteremshwa kwa Qurani.
Kwa ilivyokuwa mwezi huu ndio bora wa miezi yote, hivyo basi mema yafanywayo ndani yake yanakuwa ni bora na yanalipwa ziada kuliko miezi mengine. Hivyo basi inatakiwa kwa muislam kujibidiisha katika kufanya mema na kuepuka mabaya hasa awapo katika mwezi huu mtukufu. Baadhi ya mambo tutakiwayo kuyatekeleza:
1. Kusoma Qurani
Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala);
“Mwezi wa Ramadhani ambayo imeteremshwa ndani yake Qur-an hali ya kuwa ni uongofu kwa watu …………"
Subscribe to:
Posts (Atom)