Friday, July 26, 2013

HUYU NDO MSANII ALIYETANGAZA KUMPORA MUME WA AUNT EZEKIEL... !!!

KATIKA hali isiyo ya kawaida msanii anayechipukia katika filamu za Kibongo, Isabella Fransis ‘Vai wa Ukweli’ anamtafuta ubaya gwiji katika tasnia hiyo, Aunt Ezekiel kwa kusema anamtamani mumewe.

Vai wa Ukweli bila ya kupindisha maneno amedai kuwa hapati usingizi kutokana na kumzimia Sunday Demonte ambaye ni mume wa Aunt.


Akizungumza na mwandishi wetu, Vai alisema ili kuonesha kuwa anachokisema kinatoka moyoni mwake, amekata vipande vya picha za Dimonte na kuvibandika chumbani kwake.

 “Kusema ukweli nampenda sana Sunday na sijaanza kumpenda leo wala jana kwani namfahamu tangu zamani alipokuwa Kariakoo,” alisema Vai.

Msanii huyo chipukizi alisema anamuonea wivu Aunt kwa kuamini kuwa anafaidi sana kwa kuwa na mwanaume huyo.
 

Kwa upande wake Aunt alishangazwa na taarifa hizo na akaomba atafutwe baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ajue cha kufanya.

FABREGAS AFUNGUKA, ATAMANI KUJIUNGA NA MOYES, VAN PERSIE OLD TRAFFORD


Uncertain future: Cesc Fabregas could leave Barcelona for Manchester United 
Haijulikani hatima yake: Cesc Fabregas  anaweza kujiunga na Manchester United
Lakini ukweli ni kwamba  Fabregas amewaambia maswahiba wake wa England kuwa anataka kuondoka Camp Nou, na hii inawapa moyo zaidi kumnasa.

Inafahamika kuwa Fabregas amevutiwa na ahadi nzuri ya kucheza muda wote katika kikosi cha United na anapenda kujiunga na nyota mwenzake wa zamani wa Asernal, “Hakunaga” Robin Van Persie ambaye kwa sasa ndio roho ya ushambuliaji ya pale Old Trafford.

MZEE SMALL ANAENDELEA VIZURI KIASI,LAKINI BADO ANAHITAJI MSAADA WETU WADAU


Taarifa ya Mrejesho : Hali ya Msanii nguli wa maigizo hapa nchini Tanzania, Ndg
Said Bin Wangamba almaarufu kama Mzee Small inaendelea vizuri, na
ANASHUKURU sana kwa wale wote wanaomkumbuka katika kipindi hiki kigumu
cha maradhi. Kwa sasa anaweza kujikongoja taratibu mwenyewe.,

Anaendelea na mazoezi ya kila siku, na kubwa ni dozi ya dawa kwa ajili  ya kumsaidia kuondoa uvimbe uliogundulika miezi kadhaa iliyopita,  kichwani mwake ambapo dozi moja tu inagharimu takribani 30,000TZS pamoja
na mahitaji mengine ya lazima ya kila siku,
 Kwa yeyote atakaeguswa  tafadhali unaweza kuwasiliana na Mzee wetu kupitia, M-PESA kwa kutumia  namba ya Said Ngamba (Mzee Small) 0754647265 na TIGO PESA kwa kutumia  namba ya mkewe 0658111311,

Changamoto: Ni Wakati MUAFAKA Sanaa kuwa Ajira Rasmi na yenye MAPATO STAHIKI, Alituchekesha na kutuondolea uchovu kwa kipaji chake, nasi tumkumbuke na kumuenzi,
 
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma

MAJANGA MADANGURO YA MAKAHABA YAZIDI KUFUMULIWA....!!!


 
 Hili ni sakata la  kikongwe mmoja anayedaiwa kumiliki idadi kubwa ya madanguro katika uwanja wake na kuwapangisha makahaba katika eneo maarufu kwa jina la Kijiji cha Makahaba.
Mwandishi wetu alipokea ujumbe mfupi ulioelezea ufuska unaofanywa na mabinti ambao hupewa eneo na kujenga vibanda kisha kujiuza kwa bei chee katika kijiji hicho maeneo ya Kigamboni jijini Dar.


Bada ya simu hiyo, uchunguzi wetu  ulibaini kwamba, eneo hilo linalofanyiwa ufuska huo linamilikiwa na kikongwe aliyejitambulisha kwa jina la mzee Matutu akidaiwa kuendesha maisha kwa biashara hiyo ya madanguro.
 
Baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuwa ni kweli jambo hilo linafanyika eneo hilo,waandishi walivamia eneo la tukio wakiwa na mjumbe wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina la Abbas na kujionea madanguro yaliyojengwa kwa mstari ambapo milango yake iliachwa wazi huku ndani wakionekana mabinti wakiwa wamejilaza kihasarahasara wakiwatega wateja wanaopita katika mtaa huo.

MAAJABU: BINTI ALIYEZALIWA BILA MACHO WALA PUA ATAKIWA KUTOA UBAVU WAKE ILI AFANYIWE UPASUAJI...!!!

Msichana Brave Cassidy Hooper (17) kutoka Charlotte, Kaskazini mwa Carolina Marekani aliyezaliwa bila pua wala macho anategemea kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kurekebisha uso wake.

u-4
Brave anategemewa kufanyiwa upasuaji huo (July 31) mwaka huu ambapo inategemewa sehemu ya mfupa utaondolewa katika ubavu wake kwaajili ya kutumika kutengeneza paji la uso wake, mfupa huo utasaidia kama kiunganishi cha pua mpya atakayowekewa.

IRENE UWOYA AREJEA NCHINI KUTOKA KWA MSWATI - AMEAIDIWA MAMBO MAKUBWA

 
Mwigizaji Irene Uwoya amerejea nchini toka nchini Swaziland alipokuwa kwa takribani wiki tatu.
Irene Uwoya aliyerejea nchini leo hii amerejea na salamu toka nchini Swaziland alizoziandika kupitia ukrasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii alisema…
 
“Mswat anawasalinmu sana! Nahiv karibun atatinga hapa nakanipa kibali chakufanyya move na ful suport...I wl prove u wrong...try me”
 
Akimaanisha, amerejea nchini na Mswati amnawasalimia sana na amesema atakuja nchini hivi karibuni na amenipa kibali cha kufanya Filamu na atanisaidia kwa kila kitu. Nijaribu nitakuthibitishia kuwa umekosea (Kwa Kiswahili fasaha).
 
Bado tunamtafuta Irene amabye namba yake ya simu haipatikani kujua kama kauli hii ni ya kweli au anawatania tuu mashabiki wake.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 26, 2013


DSC 0095 1cb01
DSC 0096 51ada

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...