Ngassa alifunga bao la kwanza kwa
shuti kali la umbali wa mita 20, baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki
wawili wa JKT Ruvu, wakati bao la pili alifunga kwa kichwa akiunganisha
mpira wa kurushwa na beki Mbuyu Twite.
Pamoja na kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nyuma kwa 2-0, lakini JKT Ruvu ndiyo waliocheza soka ya kuvutia ya pasi za hapa na pale, huku Yanga wakitumia mashambulizi ya haraka kwa mabeki kupeleka mipira pembeni, ambako mawinga wanatia krosi washambuliaji wagombanie goli.
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na staili yao kushambulia kutokea pembeni, huku JKT Ruvu wakionekana kuanza kupoteza mwelekeo na kutoa mwanya zaidi wa kushambuliwa.
Beki Oscar Joshua aliipatia Yanga bao la tatu dakika ya pili ya kipindi cha pili, akiunganisha kona maridadi iliyochongwa na kiungo Simon Msuva.

Kona hiyo ilitokana na kazi nzuri ya kipa wa JKT Ruvu, Sadick Mecks aliyepangua shuti kali la kiungo wa Yanga, Frank Domayo.