KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi mk o a n i Ki l ima n j a r o ,
wamelazimika kutumia mifuko ya plastiki (malboro) kujikinga na maambukizo ya
ugonjwa wa Ukimwi, huku wengine wakichangia kondomu, jambo ambalo ni hatari na
linaelezewa kuwa moja ya chanzo cha ongezeko la maambukizo mapya ya ugonjwa huo
mkoani humo.
Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizo ya
ugonjwa wa Ukimwikatika Mkoa wa Kilimanjaro, kimepanda kutoka asilimia 1.9
mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 3.8 mwaka 2011/2012.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali, linalojihusisha na mapambano
dhidi ya Ukimwi mkoani Kilimanjaro (KACA) Faraji Swai alisema wananchi wa maeneo
ya vijijini wako hatarini zaidi kupata maambukizo ya ugonjwa ya ukimwikutokana
na kwamba wengi bado hawajafikiwa.
Alisema Shirika la Kacakatika utoaji elimu ya mapambano
dhidi ya Ukimwi kwa jamii, wamefika katika baadhi ya vijiji mkoani Kilimanjaro
na kuwakuta wananchi wakitumia mifuko ya plastiki (malboro) kama kinga ya
kujikinga na maambukizo ya Ukimwihuku wengine wakichangia kondomu jambo ambalo
liliwashangaza.