MSHAMBULIAJI hatari wa Mbeya City
fc, Mwegane Yeya amefurahishwa na kitendo cha kuitwa katika kikosi cha
timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi, Mart
Nooij.
Akizungumza na mtandao huu,
Mwegane amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kupata nafasi hiyo
kwasababu Tanzania ina wachezaji wengi wenye viwango vya hali ya juu,
lakini amechaguliwa yeye.
“Hii ni nafasi nyingine muhimu
kwangu. Niliwahi kuitwa katika kikosi cha Young Future Taifa Stars na
Kim Poulsen, lakini sikufanya vizuri kwasababu nilikuwa majeruhi.
Naamini kwasasa nitaitumia vizuri nafasi hii”. Alisema Mwegane ambaye ni
hatari kwa kufunga magoli ya kichwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mwegane aliongeza kuwa kuitwa na
Nooij ni ishara ya kukubali kazi yake, hivyo anajiona mwenye wajibu
mkubwa wa kuisadia Stars kuelekea mchezo muhimu dhidi ya Msumbiji.
Nyota huyu wa Wagonga Nyundo wa
Mbeya ni miongoni wa wachezaji wa Kikosi cha Taifa Stars kinachotarajia
kuingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya
Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa
shirikisho la soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura Mgoyo, Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku
tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa
programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka
huu.
Wachezaji wanaotakiwa kuripoti
kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin
Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar
Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Frank
Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna
Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin
Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment