Maafisa wa polisi nchini Brazil
wametumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika siku
ya pili ya mgomo wa wafanyikazi wa sekta ya uchukuzi ambao umesababisha
uhaba mkubwa wa usafiri wa uma katika mji wa Sao Paulo.
Takriban nusu ya vituo vya treni vilifungwa na
kusababisha msongamano mkubwa wa watu katika barabara za mji huo mkubwa
ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe la dunia kuanzia alhamisi
ijayo.Wafanyakazi hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi.
Awamu nyengine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo utaendelea kwa mda usiojulikana. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment