Baadhi
ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa
za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo
umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es
Salaam
Mjane wa
Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca
Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya
kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote
zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za
kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara
Mjane wa
Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust
(GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa
Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mjane wa
Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca
Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akisalimiana na baadhi ya viongozi
mbalimbali kutoka mkoani Mara.
Baadhi
ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara wakizungumzia namna
walivyonusurika kufanyiwa vitendo vya kikatili (kukeketwa). Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akiwasikiliza.
Viongozi
mbalimbali wastaafu wa Serikali, viongozi wa dini Mkoa wa Mara,
wawakilishi wa wanafunzi Mkoa wa Mara wakiwa katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike
zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Baadhi
ya viongozi wa mashirika mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa
kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa
mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca
Michel leo jijini Dar es Salaam.
Mjane wa
Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca
Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akizungumza kabla ya
kuzindua rasmi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike
zitakazoendeshwa mkoani Mara
Baadhi
ya wanafunzi wakiangalia ujumbe mfupi uliotumwa kwa simu zote
zilizosajiliwa kwa njia ya simu za kiganjani na Mjane wa Hayati Nelson
Mandela, Bi. Graca Michel kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya
Jamii Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba kupinga ndoa za utotoni kwa
watoto wa kike.
Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Moja ya
kikundi cha maigizo kikionesha igizo namna mtoto wa kike anavyokabiliana
na changamoto za unyanyasaji kutoka kwa jamii katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike
JUMLA
ya wasichana wenye umri mdogo wapatao 984 wameolewa na kukatishwa
masomo huku wasichana wengine 1,628 wakikeketwa wilayani Tarime, Mkoa wa
Mara ikiwa ni miongoni mwa vitendo vya kikatili ambavyo amekuwa
akifanyiwa mtoto wa kike baadhi ya maeneo nchini Tanzania. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment