Usitishaji wa muda mrefu wa mapigano umekubaliwa kati ya Israel na wapiganaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
Kusitishwa kwa mapigano hayo, kumehitimisha wiki
saba za vita vilivyosababisha vifo vya watu zaidi ya 2,200, wengi wao
wakiwa Wapalestina. Mazungumzo hayo yalisimamiwa na Misri na yalianza
kutekelezwa jana moja usiku.Maafisa wa Israel wamesema Israel italegeza vikwazo ilivyoiwekea Gaza ili kuruhusu misaada na vifaa vya ujenzi kuingia Gaza.
Msemaji wa serikali ya Israeli, Mark Regev amesema: "hebu tuwe na matumaini kwamba mpango huu wa kusitisha mapigano utaheshimika"
Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja katika masuala yenye utata, ikiwa ni pamoja na wito wa Israel wa kuyataka makundi ya wapiganaji yanapokonywa silaha, yataanza mjini Cairo katika kipindi cha mwezi mmoja. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia amepongeza mpango huo wa kusitisha mapigano. Lakini katika taarifa kupitia kwa msemaji wake, Bwana Ban ameonya kuwa "jitihada yoyote ya amani ambayo haishughulikii chanzo halisi cha mgogoro, itafanya kazi kidogo kuliko kutengeneza mzunguko mwingine wa ghasia".
Hatua ya kusitisha mapigano imekuja huku Israel na Wapalestina wakiendelea kushambuliana.
Kombora la dakika ya mwisho ya makabiliano kutoka Gaza limemuua raia wa Israel na kuwajeruhi wengine sita katika Barazala la Jimbo la Eshkol, wafanyakazi wa afya wameiambia BBC.
Maafisa wa Palestina wamesema pendekezo la Misri la kusitisha mapigano linataka kumalizwa kwa uhasama kusiko na kikomo, kufunguliwa haraka kwa mipaka ya Gaza na Israel na Misri na kuongezewa ukanda wa uvuvi katika bahari ya Mediterani..
Tangazo la kusitisha mapigano lilishangiliwa na Wapalestina katika mji wa Gaza.
Kabla ya kuanza utekelezaji wa mpango huo, majengo marefu mjini Gaza yalishambuliwa na makombora zaidi yalipiga Israel.
Mwezi mmoja baadaye Israel na vikundi vya Wapalestina vitajadili ujenzi wa bandari na uwanja wa ndege huko Gaza na kuwaachilia huru wafungwa 100
Israel na Misri pia zimesemekana kutaka kuhakikishiwa kuwa silaha hazitaingizwa Gaza kwa njia ya magendo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment