Filikunjombe mwenye shati la kijani akishirikiana na wananchi kufukia nguzo
Vijana wa TANESCO wakiwa kazini
Kazi na dawa Filikunjombe akiwa na kihifadhia chakula (Hot port) lenye karanga baada ya njaa kumkabili
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Filikunjombe akichimba shimo
Shimo hili lilifika futi sita hilo Filikunjombe akishirikiana na wananchi hadi kuhakikisha nguzo zinasimama
Wanawake wakazi wa Lupingi wakikata miti nili nguzo ziendelee kupita
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
WANANCHI wa kijiji cha Nindi Kata ya
Lupingu wilayani Ludewa wamekubali kuruhusu maeneo yao kutumika
kupitisha nguzo za umeme zinazowekwa hivi sasa na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) bila ya kuidai serikali fidia.
Uamuzi wa wananchi hao kuruhusu
kutumika kwa maeneo yao umeadhimiwa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Ludewa,
Deo Filikunjombe wakati alipoongoza wananchi hao wa kijiji cha Mtumbati
kufyeka miti iliyopo kwenye mashamba yao kwa ajili ya kuchimba mashimo
ya kuweka nguzo za umeme.
"Iwapo wananchi hao wangekuwa kama
wale wa mijini ama mikoa mingine ambao wamekuwa wakikwamisha miradi
kuanza kwa wakati kutokana na kudai fidia kwa kila kitu, basi
isingewezeka umeme kufika Lupingu, ungechukua muda mrefu zaidi, hasa
kutokana na wingi wa miti,mashamba ya mihogo na mali nyingine ambazo
zingepaswa kufanyiwa tathimini kabla ya kuondolewa," alisema
Filikunjombe.
"Tunamshukuru mbunge kwa jitihada zake
hizi anazozionyesha hivi sasa kwenye jimbo letu, tumeshirikiana kwa
pamoja kufanya kazi na yeye kwa ajili ya kufyeka na kuchimba mashimo,
tumekubaliana hatuoni sababu ya kudai fidia mashamba yetu yalipwe na
serikali," alisema Hapiness Kayombo mkazi wa Mtumbati.
Naye Otilia Lukuu mkazi wa Nindi
alimpongeza Mbunge Filikunjombe kwa kuwaletea maendeleo ya haraka kwenye
kijiji chao hicho, ambapo alidai awali hali ya mawasiliano ya barabara
kutoka kijiji cha Nindi kwenda Ludewa ilikuwa ni changamoto kubwa na
kwamba hivi sasa usafiri wa basi na gari ndogo umekuwa ukitumiwa na
wakazi wa Lupingu wanaofanya biashara ya dagaa na samaki kwenda kuuza
mjini Ludewa.
"Tunafurahi kupata hivi sasa barabara
ya uhakika ya kupitisha magari, na vilevile ujio wa umeme kwenye kijiji
chetu, kila mkazi atakuwa na uhakika wa kupata umeme, hatuoni sababu ya
kudai fidia kwenye mashamba yetu," alisema Lukuu.
Mbunge Filikunjombe akiwa kwenye
kijiji cha Nindi aliwapongeza wananchi wa kijiji vya Nindi, Mtumbati na
Lupingu kuruhusu maeneo yao hayo kutumika kupitisha nguzo za umeme
kutoka mjini Ludewa kwenda Kata ya Lupingu bila ya kudai fidia yoyote,
jambo ambalo litasaidia kuleta maendeleo makubwa kwenye kata hiyo pindi
umeme huo utakapowashwa.
Filikunjombe alisema jitihada
anazozifanya kwenye jimbo lake la Ludewa ni sehemu ya kutimiza ahadi
zake kupitia Ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi (CCM), ambayo
iliahidi kufikisha umeme kila kaya kwa lengo la kuchochea maendeleo kwa
haraka katika maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa hayapati nishati
hiyo ya umeme.
Mbunge huyo ambaye alishirikiana na
wananchi hao kuchimba mashimbo, kufyeka miti na kubeba nguzo za umeme,
alisema ameridhishwa na kasi inayofanywa na wananchi hao ya kujitolea
nguvu zao kuchimba mashimo na kusogeza nguzo katika mashimo hayo,kuwa ni
wazi mradi huo wa umeme utakamilika kabla ya mwezi Desemba mwaka huu.
Filikunjombe alisema, wakati akiingia
madarakani mwaka 2010 ni Kijiji kimoja pekee cha jimbo hilo la Ludewa
ambacho kilikuwa na umeme wa mafuta, lakini hivi sasa zaidi ya vijiji 10
tayari vimepata umeme na kwamba jumla ya vijiji 49 vipo kwenye mpango
huo wakufikiwa na mradi wa umeme huo ambao unatekelezwa kwa nguvu za
serikali ya Tanzania, Swedeni na Kanisa na Katoliki Dayosisi ya Njombe.
Akizungumzia kasi ya usambazi wa nguzo
za inayoendelea hivi sasa ya kupeleka umeme kwenye Kata ya Lupingu,
Kaimu Meneja wa Tanesco wilayani Ludewa, Ramadhani Mwanga alisema
wanatarajia kuanza kuweka nyaya za umeme kutoka Ludewa hadi kijiji cha
Nindi ndani ya wiki mbili zijazo.
"Tupo mbioni kuwasha umeme kwenye
vijiji hivi, lakini tumekuwa tukifanya kazi kwa kasi kuhakikisha hadi
kufikia mwezi Desemba umemeuwe umeshawaka kwenye vijiji vyote vilivyopo
ndani ya kata ya Lupingu," alisema Mwanga. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mathias Canal
No comments:
Post a Comment