Kabla ya mkutano wao wa ana kwa ana katika mji mkuu wa Belaruse, Minsk, viongozi hao wawili pia walishiriki katika mazungumzo na afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton.
Mwanadiplomasia Ashton ameyaelezea mazungumzo yaliyowashirikia viongozi mbalimbali wa Ulaya kuhusu mgogoro wa Ukraine kuwa una mwelekeo"sahihi".
Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani zimeiwekea Urusi vikwazo vya uchumi kwa kushindwa kuwadhibiti waasi. Zaidi ya watu 2,000 wameuawa katika mapigano kati ya majeshi ya Ukraine na waasi katika majimbo ya Donetsk na Luhansk.
Majimbo hayo mawili yamejitangazia uhuru kutoka Kiev kufuatia hatua ya Urusi ya kujinyakulia eneo la kusini la Crimea kutoka Ukraine mwezi March 2014.
Mazungumzo kati ya Bwana Poroshenko na Bwana Putin yalidumu kwa takriban saa mbili bila kuruhusu vyombo vya habari. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment