Mahakama nchini India imemuhukumu
nyota muigizaji wa sinema za Bollywood Salman Khan, kifungo cha miaka
mitano jela kwa kuua aina mojawapo ya swala ambao ni adimu kupatikana
duniani mwaka 1988.
Mahakama hiyo iliyoko Jodhpur imemtoza faini ya rupia 10,000 ($154; £109) kwa kosa hilo.
Amepelekwa korokoroni na anatarajiwa kusalia huko kwa muda.
Khan aliwaua swala wawili kwa jina blackbucks, ambao hulindwa na kuhifadhiwa, Magharibi mwa jimbo la Rajasthan alipokuwa akiigiza filamu yake.
Waigizaji wengine wanne walioshiriki naye uigizaji kwenye filamu
hiyo, waliokuwa wamehukumiwa kwa kosa hilo na mahakama ya awali,
walisamehewa. Khan (52), anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama ya juu.
Hii
ni kesi ya nne iliyowasilishwa dhidi ya mwigizaji huyo inayohusiana na
uwindaji haramu wa wanyama wakati walipokuwa wakiigiza filamu ya Hum
Saath Hain mwaka 1988. Amesamehewa makosa matatu.
Mwaka
2006, mahakama ilimuhukumu mwigizaji huyo kwa makosa mawili ya uwindaji
haramu na kumuhukumu miaka mitano jela. Mahakama ya juu ya Rajasthan
ilitupilia mbali uamuzi huo mwaka 2007 na mwaka 2016 ikampa msamaha.
Serikali imekata rufaa dhidi ya uamuzi huo uliotolewa na mahakama kuu. Kesi halisi ya uwindaji dhidi yake iliwasilishwa na jamii ya Bishnoi ambao wanawaheshimu na kuwaabudu swala hao aina ya blackbuck.
No comments:
Post a Comment