Mjumbe mwingine wa Bunge la Katiba
kutoka Kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) jana alionekana
kwenye Viwanja vya Bunge na alisaini za mahudhurio.
Mjumbe aliyeonekana jana, Leticia Nyerere wa viti
maalumu, Chadema, anafanya idadi ya wajumbe waliotinga kwenye viwanja
hivyo hadi sasa kufikia watatu baada ya Chiku Abwao (viti maalumu
Chadema) kuonekana juzi na Clara Mwatuka (viti maalumu CUF) kuonekana
Jumapili.
Nyerere hakuwa akihudhuria vikao baada ya Ukawa kutangaza kususia Bunge mwezi Aprili na jana hakupatika kuzungumzia suala hilo.
Kuonekana kwa mjumbe hao kunaweza kutafsiriwa kuwa
ni kubomoka kwa ngome za Vyama vya Chadema, NCCR na CUF vinavyounda
umoja huo kwani tangu awali walikubaliana kutoshiriki shughuli za Bunge
hadi pale watakapofikia makubaliano ya hoja zao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Msimamo wa chama hicho chini ya viongozi wao ni
kutohudhuria shughuli za Bunge Maalumu la Katiba hadi kutakapokuwa na
mwafaka wa mwenendo wa shughuli za chombo hicho, ambacho jana
kiliendelea na vikao vya kamati kujadili sura 15 za Rasimu ya Katiba.
Ukawa wanadai CCM imepora mawazo ya wananchi na
kwamba kuna mpango wa kuchakachua rasimu iliyotolewa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba na kuingiza mambo yenye masilahi kwa chama hicho na
Serikali yake.
Vyama vinavyounda Ukawa vinadai kuwa kuzungumzia
muundo wa Muungano wa serikali mbili ni kuchakachua maoni ya wananchi
ambao walitaka muundo wa serikali tatu kama ilivyo kwenye Rasimu ya
Katiba.
Bunge jana lilikutana katika kamati zake 12
zilizotawanyika katika kumbi mbalimbali kwa ajili ya kupitia sura 15 za
rasimu ya Katiba ingawa wajumbe wengine walilazimika kuanzia safari zao
bungeni ili waweze kujisajili.
Mwenyekiti wa Kamati namba tano ambayo Nyerere ni
mjumbe, Hamad Rashid Mohamed alisema mjumbe huyo hakuwa amefika katika
kikao cha jana ambacho pia kilifanyika Dodoma Hoteli.
Kuhusu mwenendo wa kikao cha kamati yake, Mohamed
alisema hadi jana mchana walikuwa wamekamilisha kupitia sura ya pili na
kwamba jioni walitarajia kuifanyia kazi sura ya tatu.
Kuhusu changamoto ya muda, Mohamed alisema: “Hiyo
ndiyo hali halisi na tukiweza tutapiga kura kupitisha ibara hizo leo
(jana), kama tukishindwa basi tutapiga kura kesho (leo) ili mradi
tutumie muda ambao upo tufanye kazi kwa ufanisi.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment