Manchester City wameshindwa kufika
katika fainali za kwanza za klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) baada ya
kutolewa na mabingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid katika mchezo
uliokua wa kuvutia tena wa aina yake. Walichapwa 1-0.
Baada ya
kutokuwa na ushindi wowote katika mzunguko wa kwanza, Real Madrid
walianza kuongoza kipindi cha kwanza kufuatia mpira wa krosi uliopigwa
na Gareth Bale kumbabatiza kiungo wa City Fernando na kuingia nyavuni.
Real waliutawala mchezo huku mpira wa kichwa uliopigwa na Bale ukigonga
mwamba na baadaye mlinda mlango wa City Joe Hart akiondoa mikwaju ya
Luka Modric na Cristiano Ronaldo.
Klabu hiyo ya Uingereza ilikuwa ikihitaji bao moja muhimu la ugenini
hususan katika dakika za lala salama kuelekea fainali,lakini hilo
halikuweza kufanikiwa licha ya kushangiliwa na mashabiki wake wapatao
4,500.
Madrid walipata wakati mgumu kidogo pale mkwaju mkali wa
Sergio Aguero ulipogonga nyavu za juu za lango la Madrid. Real sasa
watakutana na Atletico katika uwanja wa San Siro tar 28 Mei, hii ikiwa
ni kama marudio ya fainali za mwaka 2014 ambapo Real walishinda kwa
mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza.
No comments:
Post a Comment