Friday, September 06, 2013

"TATIZO LA UJENZI HOLELA NI KUBWA JIJINI DAR" SERIKALI

majengo_234e1.jpg
Serikali imekiri kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa ujenzi ambao haufuati kanuni, taratibu na sheria zilizopo hususan katika Jiji la Dar es Salaam.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia ambaye alisema kuwa Serikali imeliona jambo hilo na sasa inapitia sheria upya ili kurekebisha hali hiyo.
Waziri aliyataja maeneo ambayo yanahusika na ukiukwaji ni pamoja na utoaji wa vibali vya ujenzi pamoja na ubadirishwaji wa matumizi ya ardhi na uvamizi wa viwanja vya wazi.
Maeneo mengine ni ukiukwaki wa maadili ya kitaaluma usiozingatia sheria ya mwaka 2007 ya sheria ya mipango miji na kanuni za udhibiti wa ujenzi.

Alikuwa akijibu swali la Muhammed Amour Chombo (Magomeni,CCM) aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kukomesha utovu wa nidhamu dhidi ya waliopewa dhamana ya kusimamia sheria za mipango miji katika kuruhusu ujenzi.

Waziri alisema kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kisheria na kinidhamu dhidi ya watendaji wanaoshindwa kutimiza sheria, kanuni na taratibu za mipango miji ya ujenzi.
"Serikali hivi sasa inapitia sheria ya mipango miji na taratibu za utoaji wa vibali vya ujenzi na usimamizi hasa katkia Jiji la Dar es Salaam ili kuboresha na kuhakikisha kwamba zoezi zima la utoaji wa vibali vya ujenzi na udhibiti wa kutosha," alisema Ghasia.
Alisema Serikali katika mwaka 2013/14 imeanza kutekeleza mpango makakati utakaoimarisha usimamizi na udhibiti wa takwimu za kijiografia za matumizi ya ardhi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...