Arsene Wenger
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameeleza furaha yake baada ya klabu hiyo kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameeleza furaha yake baada ya klabu hiyo kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili.
Wenger amesema alifurahishwa sana na uchezaji
wa timu yake na kueleza kuwa walishangaza Manchester United kuanzia
mwanzo wa mechi.
“Kuanzia kwa Petr Cech hadi kwa Theo Walcott wote
walicheza vyema. Nimenoa timu nyingi kali lakini hakuna hata moja
iliyoweza kucheza mechi 60 katika kiwango sawa. Lazima ukubali kwamba
sisi ni binadamu,” alisema.
“Tuko kwenye kinyang’anyiro (cha
kushindania taji), tuko alama mbili nyuma ya viongozi Manchester City na
natumai matokeo ya leo yatatupa imani ya kuendelea kupigania taji.” Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Arsenal
walipata ushindi kupitia mabao mawili ya nyota wa Chile Alexis Sanchez
na Mjerumani Mesut Ozil, mabao yote yakifungwa kipindi cha kwanza kwenye
mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Emirates.
Kwa meneja wa Manchester United Louis Vvan Gaal, ilikuwa vigumu kukubali matokeo hayo.
„Tulianza
vibaya sana, bila kuonyesha ari ya kushambulia na kutaka kushinda.
Ilikuwa mara ya kwanza kwangu kushuhudia hilo katika timu yangu.
Sikulitarajia hili,” amesema.
„Unapoipatia timu kama Arsenal mianya tele uwanjani ya kusakata gozi, basi unajua kwamba lazima utashindwa.”
Arsenal
na Manchester United sasa zinatoshana alama ingawa Arsenal wako mbele
wakishikilia nambari mbili kwenye jedwali kwa wingi wa mabao.
Timu
hizo zitarudi mawindoni wiki mbili zijazo mnamo Oktoba 17, baada ya
mapumziko ya wiki mbili ya mechi za kimataifa, ambako United watakutaka
na Everton uwanjani Goodison Park nao Arsenal wawe ugenini Watford. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment