Mshambuliaji wa England Wayne Rooney akijiandaa kuandika historia ya kuwa miongoni mwa wachezaji walioichezea timu yao ya Taifa michezo 100 na zaidi.
Mara nyingi wachezaji wa England wanapokuwa wamecheza michezo 99 huwa na utamaduni wa kwenda kwenye shule zao na kupigia picha na jumla ya wanafunzi 99
England inajiandaa kucheza mchezo wa kufuzu fainali za Euro 2016 dhidi ya Slovenia mwishoni mwa juma hili kwenye dimba la Wembley,huenda Rooney ambaye pia ni nahodha wa kikosi hicho akatimiza mchezo wa 100 siku iyo na kuwa mchezaji wa 9 kuichezea England michezo 100.
Hiyo ndio ilikuwa sababu ya Rooney kurejea kwenye shule yake ya Primary, Our Lady and St Swithin’s Catholic Primary School iliyopo kwenye jiji la Liverpool.
siku ambayo DAVID BECKHAM alikuwa nacheza mchezo wa 100 alikabidhiwa kofia ya dhahabu……..
LAMPARD pia alikabidhiwa kofia ya dhahabu kama ilivyo kawaida………..
No comments:
Post a Comment