Meneja
wa Tigo Bw. William Mpinga akielezea jinsi kampuni ya Tigo ilivyoshinda
nafasi ya nane duniani yenye mahusiano ya karibu na wateja wake kwenye
mtandao wa kijamii wa Facebook.
Tigo
Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa makampuni bora zaidi duniani yenye
mahusiano ya karibu na wateja wake kwenye mtandao wa kijamii wa
Facebook. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la
SocialBokers tarehe 7 February, 2013 ambalo lilifanya utafiti wa
makampuni 10 bora zaidi duniani yenye uhusiano wa karibu na wateja
kwenye mitandao ya jamii kwenye kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka
2012. Tigo Tanzania ndiyo shirika pekee la simu kutoka kanda ya Kati,
Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika lililofikia viwango hivyo
vilivyojumuisha makampuni yote bora duniani.
Mitandao
ya kijamii inajitokeza kuwa njia rahisi zaidi kwa wateja mbali mbali
kupata taarifa, kuomba misaada na kuelimishwa kuhusu bidhaa mbalimbali,
na makampuni yaliyo na uhusiano bora na wateja wao na yenye uwezo
mkubwa yamechukua fursa hii kuboresha mahusiano na kuwa karibu na
wateja wao. Mitandao hii mikubwa ya kijamii duniani kama vile Facebook,
hutoa njia m-badala na iliyo bora kwa mashirika yaliyozidiwa ki-huduma
na hivyo kutoa fursa kwa watu wa tamaduni mbali mbali kushirikishana
kujadili na kueleweshana.
”
Tigo Tanzania imeibuka kuwa namba 8 duniani kote kwenye tafiti hizi
kutokana na kujikita vilivyo kwenye kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora
na za kujitosheleza kwa wateja wake.Tunathamini sana wateja wetu na
tunahakikisha kuwa tuko pamoja nao wakati wote kila wanapotuhijati.
Maendeleo ya kiteknolojia na dijitali yamewezesha kuwepo kwa mijadala
mingi kila wakati kwenye mitandao ya kijamii. Tigo kama Kinara wa
uvumbuzi wa bidhaa za mawasiliano inatazama changamoto hii kama fursa
ya kujiweka karibu zaidi na wateja na kushirikiana nao kwa ukaribu
zaidi. Kila tunachofanya Tigo ni kwa ajili ya wateja wetu, hivyo
kutambuliwa huku ki-dunia ni fahari kubwa sana kwetu” alisema Ndg.
William Mpinga Manager brand ya Tigo.
Kwa
mujibu wa shirika la SocialBoker, utafiti wa mashirika yanayojituma
zaidi kijamii kwa kipindi cha mwezi Oktoba na Desemba, 2012, umeonyesha
kuwa mashirika huwajibika na kujibu hoja kutoka kwa wateja wao haraka
zaidi kwenye kurasa za Facebook. Hoja iliyokuwa inajibiwa kwa wastani
wa masaa 21 miezi ya nyuma sasa makampuni yanaweza kujibu kwa kipindi
cha masaa 19.5 tu kuelekea mwishoni mwa 2012. Shirika la simu la Tigo
Tanzania limepata asilimia 87.30% kwa kujibu hoja ndani ya masaa 28.
“Tigo
Tanzania mbali ya kujibu hoja za wateja kwenye mitandao ya kijamii
inahakikisha kuwa inafanya hivyo kwa ufanisi zaidi kila wakati. Kwa
kuwa mstari wa mbele kwenye kutambua hilo tumefanikiwa kupata heshima
hii kubwa. Tutazidi kuongeza ubunifu ili kuboresha huduma na bidhaa
zetu, na tunatambua kwamba, ili kutoa huduma stahili, ushiriki wa wateja
wetu ni nyenzo muhimu sana. Tumepata mafanikio makubwa tuliyonayo na
kufika hapa tulipo leo kwa kuupa utoaji wa huduma bora kipaumbele, na
kwa
heshima hii kubwa, tunaahidi kuwa tutajikita kuhakikisha tunaendelea
kutoa ufumbuzi wa mawasiliano uliobora zaidi jambo litakalomfanya kila
mteja wetu kutabasamu.” alihitimisha Ndg Diego Gutierrez, Managa wa
Tigo.
Socialboker
ndilo shirika linaloongoza duniani miongoni mwa mashirika yanayofanya
tafiti na kutoa takwimu kuhusu mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter,
Google+, LinkedIn na You tube. Kwa njia hii inasaidia makampuni uwezo
wa kampeni za kijamii za makampuni yao. Tafiti za hivi karibuni
zinajumuisha taarifa za Desemba 2012 za ‘Global Social Media Report’
ambapo utafiti mkubwa ulifanywa ukihusisha idadi ya kurasa za Facebook
na watumiaji wake kidunia katika mataifa ya Marekani, Uingereza na
Brazili. Mengine ni Azerbaijan, Serbia, Mexico, Poland na El Salvador-
kwa kutaja machache.
No comments:
Post a Comment