Kauli hiyo ya tahadhari imetolewa na Mwanasheria
Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu hatua ya baadhi ya wabunge wa chama hicho kuonekana mjini
Dodoma, kunakofanyika vikao vya Bunge Maalumu la Katiba (BMK) ambalo
Ukawawamesusia kuhudhuria.
“Ni bora wawe wabunge wa mahakama kama mwenzao
(akimlenga Zitto Kabwe), kuliko kuendeleza usaliti ndani ya chama.
Tunatarajia kukaa na wenzetu kushauriana nini cha kufanya dhidi ya wote
wanaoenda kinyume na msimamo wa Ukawa,” alisema Tundu Lissu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Baadhi ya wabunge wa Ukawa hasa kutoka Chadema,
akiwamo Leticia Nyerere (Viti Maalumu), John Shibuda (Maswa Mashariki)
na Said Arfi (Mpanda Mjini) wameripotiwa kuonekana mjini Dodoma
wakijiandikisha kuhudhuria vikao vya Bunge Maalumu la Katiba tofauti na
msimamo wa vyama vinavyounda umoja huo, ambao umeahidi kutorudi bungeni
mpaka Rasimu ya Pili ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, itakapojadiliwa.
Mbali ya kuonekana Dodoma, posho imetajwa kuwa
moja ya sababu ya wabunge hao kushawishika kurudi na kuendelea na
mchakato huo wa kutunga Katiba uliogomewa na Ukawa.
“Msimamo wa Chadema kwa wasiofanya kama
ilivyopangwa na chama unaeleweka. Hatutarajii kumwogopa yeyote; awe
Nyerere, Shibuda au Arfi. Tunafahamu kuwa hawa wote wapo Dodoma na
wamesaini posho, hivyo watatueleza wakati utakapofika,” alisema Lissu.
Alisema kuwa ana uhakika kuwa Katiba Mpya haiwezi kupatikana. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment