Saturday, August 09, 2014

LIPUA LIPUA YA KAMATI ZA BUNGE MAALUMU LA KATIBA

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana. Picha na Emmanuel Herman.

Kamati za Bunge Maalumu la Katiba zilizoanza vikao vyake juzi mjini Dodoma, zimejikuta zikifanya kazi kwa kulipua kutokana na uchache wa muda uliotengwa, ikilinganishwa na ukubwa wa kazi ya uchambuzi wa ibara za rasimu ya Katiba hiyo.
Kamati hizo zimetengewa siku 14 kwa ajili ya kujadili na kuchambua sura 15 za rasimu hiyo na siku mbili za kuandaa taarifa ambazo zitaanza kuwasilishwa kwenye Bunge Maalumu, Septemba 2, mwaka huu.
 Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wamekuwa wakilalamikia ufinyu wa muda uliotengwa na kwamba kazi imekuwa ikifanyika kwa kulipua, ili kuhakikisha kwamba wanamaliza katika muda uliopangwa.
 Malalamiko hayo yanatokana na ukweli kwamba baadhi ya sura za rasimu zina ibara nyingi ambazo ni vigumu kuzijadili kwa kina, kuzifanyia marekebisho kisha kuzipigia kura kwa lengo la kuzipitisha.
 Waraka wa mgawanyo wa sura kwa siku za mjadala katika Kamati za Bunge Maalumu unaonyesha kuwa kamati zilipaswa kujadili sura ya pili na ya tatu za rasimu hiyo siku ya kwanza zilipoanza kuketi, sura hizo zina jumla ya ibara 13, kazi ambayo baadhi ya wajumbe walisema ilikuwa ni vigumu kuikamilisha kwa siku moja.
 Mwenyekiti wa Kamati namba tano, Hamad Rashid Mohamed juzi alikiri kuwapo kwa changamoto ya muda lakini akasema: “Hiyo ndiyo hali halisi, lazima tutumie muda huo ambao tumepewa na tufanye kazi kwa ufanisi”. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
 Naye Mwenyekiti wa Kamati namba nane, Job Ndugai alikiri kwamba muda ni finyu, lakini akasema ikiwa kamati zitajipanga vizuri zitaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.
 “Changamoto kubwa ni kwamba wajumbe ni wengi, kwa mfano katika kamati yangu kama wote wakihudhuria wanafikia 52, kwa hiyo sisi tulichofanya ni kuweka utaratibu wa mjadala kwamba hoja ikishazungumzwa na mtu mmoja, basi inafanyiwa kazi na siyo kurudiwarudiwa,”alisema Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
 Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema muda uliotengwa kwa ajili ya Kamati unatosha, kwani tayari wajumbe walikuwa wamesoma rasimu nzima na kuielewa kabla ya kuanza uchambuzi.
  “Kama tungesema kwamba mtu akasomee (rasimu) pale siku zisingetosha, lakini kwa sababu watu wanayo hiyo document (waraka) siku nyingi, walishaisoma na wanajua wanachotaka ni nini, basi muda huu unatosha, hata kama hatutakuwa na muda mwingi kama ilivyokuwa kwa zile sura mbili,”  alisema Hamad.
 Mgawanyo wa sura
Bunge limezigawa sura hizo za rasimu ya Katiba katika sehemu nane huku sura zinazoshabihiana zikiwekwa katika kundi moja na muda mmoja wa kujadiliwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Baada ya kukamilisha sura ya pili na ya tatu Jumatano, kamati hizo juzi zilianza kujadili sura namba nne na tano zenye ibara 37 na kazi hiyo wanapaswa kuikamilisha keshokutwa Jumatatu jioni. Ibara hizo zinahusu masuala ya haki za binadamu, wajibu wa raia, mamlaka za nchi na uraia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Kwa siku sita kuanzia Jumanne ijayo, kamati hizo zimeelekezwa kujadili sura tano ambazo ni namba 7, 14, 8, 11 na 15 ambazo zina jumla ya ibara 79 zikizungumzia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uhusiano na uratibu serikalini, utumishi wa umma, masharti kuhusu fedha pamoja na ulinzi na usalama.
 Sura ya tisa yenye ibara 37 zinazohusu Bunge la Jamhuri ya Muungano na sura ya kumi yenye ibara 36 inayohusu mahakama, kila moja imepangiwa siku moja na nusu, wakati sura ya 12 yenye ibara 11 ikizungumzia uchaguzi katika vyombo vya uwakilishi, vyama vya siasa imepangiwa siku moja ya mjadala.
 Kwa sura hizo mbili ni kwamba kamati zitajadili wastani wa ibara 23 kwa siku moja. Nyingine zilizopagiwa siku moja ni sura ya 13 yenye ibara 21 zinazohusu Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, pamoja na sura ya 16 yenye ibara sita zinazohusu masuala mengineyo.
 Itakumbukwa kuwa katika awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu, wajumbe wa Bunge hilo walitumia siku nne kujadili sura ya kwanza na ya sita zenye jumla ya Ibara 19.  Sura hizo zinazohusu masuala ya aina ya muungano, ndizo zilizua mvutano kiasi cha baadhi ya wabunge kususia Bunge hilo.
 Kutokana na hali hiyo baadhi ya kamati zimekuwa zikifanya kazi muda mrefu kiasi cha wajumbe wake kutokwenda kula mchana kama ilivyotokea juzi katika kamati namba tano.
 Mjumbe mmoja wa kamati hiyo alisema: “Hatukuweza kwenda kula maana tukitoka hapa (Hazina) kwenda mjini, muda utakwisha kabla wajumbe hawajarudi, kwa hiyo tumeamua tusitoke hadi saa kumi…” 
Kadhalika baadhi ya kamati kutokana na ufinyu wa muda zilishindwa kupiga kura siku ya kwanza kwa ajili ya kupitisha makubaliano yake na badala yake uamuzi huo kufanywa siku ya pili.
 Katika mazingira hayo kuna kila dalili kwamba baadhi ya kamati zitaomba kibali cha kufanya kazi siku za mwishoni mwa wiki ili kukamilisha kazi zake, licha ya kuwapo kwa mabadiliko ya kanuni ambazo zimeziweka kando Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...