Baada ya kuwasili hospitalini hapo saa 1:35
asubuhi, ndugu hao wakiongozwa na baba wa mtoto huyo, Rashid Mvungi
walikutana na maofisa wa ustawi wa jamii wakiongozwa na Ofisa Ustawi wa
Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungatuti wakitaka wakamzike mtoto wao
kwa kufuata imani ya dini yao ya Kiislamu.
Hata hivyo, Ngungatuti alipinga hoja hiyo akisema
suala la ndugu kuzika halina nafasi na kwamba mtoto atazikwa na ustawi
wa jamii ambao ndiyo waliokabidhiwa mtoto huyo na polisi.
“Tutamzika kiserikali kwa kuzingatia imani ya dini
yake lakini hatutawakabidhi maiti kwa namna yoyote,” Ngungatuti alisema
na kuongeza kuwa wanafanya hivyo kwa kufuata misingi ya kisheria.
Akizungumzia suala hilo Mvungi alisema: “Ndugu
zangu wanataka mtoto tupewe lakini kama sheria inakataza mimi sina neno
ila kama ingekuwa ni matakwa yangu ningependa nipewe mwanangu nikazike
mwenyewe.
Sakata hilo liliendelea mjini Morogoro ambako
baada ya mwili kuwasili, watu wanne; wanawake wawili na wanaume walifika
Ofisi za Ustawi wa Jamii na kujitambulisha kuwa ni bibi na wajomba wa
marehemu wakitaka wapewe mwili wa mtoto huyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Hata hivyo, Ofisa Ustawi wa Jamii mkoani Morogoro,
Yolanda Mkapa aliwataka waende polisi kupata kibali kabla ya kupewa
mwili huo. Baada ya majibu hayo, walitazamana na kuamua kuondoka huku
wakiacha maagizo kuwa washirikishwe katika mchakato mzima wa maziko.
Akizungumzia hali hiyo, Ngungatuti alisema hofu ya
wanandugu pengine ni kudhani kuwa rambirambi na misaada mingine
itakayotolewa itatumika visivyo dhana aliyosema si sahihi kwani marehemu
kabla ya kufikishwa Muhimbili alifunguliwa akaunti.
“Bahati mbaya amefariki na kutokana na hali hiyo
fedha ambazo zitapatikana zitaendelea kutunzwa katika akaunti hiyo na
zitawasaidia wenzake wengine wenye matatizo kama yeye wanaopokewa na
idara.”
Akizungumzia msiba huo, mlezi wa mtoto huyo,
Josephine Joel alisema amepata uchungu kwani aliamini kuwa Nasra
angerejea hali ya kawaida akisema kabla hajafariki alihangaika sana.
Historia ya Nasra
Nasra aligundulika akiwa amefichwa katika boksi na
mama yake mkubwa, Mariam Said huko Uwanja wa Ndege, Morogoro ikielezwa
kuwa alikuwa humo tangu akiwa na umri wa miezi tisa alipomchukua kumlea
baada ya mdogo wake (Mama Nasra), kufariki dunia.
Akiwa ndani ya boksi hilo ilidaiwa kuwa alikuwa akiwekewa
chakula huku akijisaidia na kulala humohumo hali iliyosababisha atapakae
kinyesi mwili mzima.
Mariam na mumewe, Mtonga Ali (30) na Mvungi
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Morogoro kujibu mashtaka
ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto huyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment