Serikali ya Brazzaville imesema kuwa watu hao walikuwa wahamiaji haramu lakini wengi wao wamekanusha hili wakisema kuwa wameteswa sana na polisi wa Brazaville. Umoja wa maaifa umetoa wito kwa Congo kukoma kuwafukuza watu hao. Hapo Jumatatu ujumbe kutoka pande zote mbili ulikutana mjini Kinshasa nchini DRC kujaribu kutafuta suluhisho.
Maelfu ya waliohamia kambi hizo za muda za DRC waliishi nchini Brazaville maisha yao yote na sasa wamepoteza kila kitu walichokuwa nacho. Wamedai kuwa polisi wa Brazaville waliwapiga, kuwabaka na hata kuwaua baadhi ya watu walioaminiwa kuwa raia wa DRC wakati wa msako wao.
Huu ni unyama
Upande wa DRC umelalamikia hatua hii na kusema kuwa Brazaville imekiuka haki za binadamu.Richard Muye ni waziri wa mambo ya ndani wa DRC. Ameambia BBC, '' Mbona sasa wanawafukuza tena kwa wingi hivi bila kujali haki zao? Wanawatesa watu wote, wake waume na hata watoto.''
Brazaville yajitetea
Lakini waziri mwenzake kutoka upande wa Brazaville Raymond Zéphirin Mboulou amekanusha kuwafukuza wakongomani 130,000. Amesisitiza kuwa ni 2000 pekee waliofukuzwa kwa lazima nchini humo, na hiyo pia ni kwasababu walikuwa wahalifu."Walifanya uhalifu wa kuchukiza. Wizi, ubakaji ukahaba na mengine. Wameharibu mitaa yetu. Na hawakaribishwi hapa tena kwasababu hao wahamiaji ndio wanaowahangaisha raia wetu usiku na mchana."
Waziri huyo ameongeza kuwa wale wengine 128,000 walioondoka walifanya hivyo kwa hiari yao. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment