KOCHA
mkuu wa Nigeria, Stephen Keshi ametaja kikosi chake cha mwisho cha
wachezaji 23 kwa ajili ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mabingwa hao wa soka barani Afrika wanaenda kushiriki
fainaili hizo kwa mara ya tano na wamepangwa kundi moja na Argentina,
Iran na Bosnia.
Wachezaji wazoefu kama Vincent Enyeama, Austin Ejide, Joseph
Yobo na Elderson Echiejile waliokuwa sehemu ya kikosi cha fainali za
mwaka 2010 nchini Afrika kusini wamejumuishwa katika orodha hiyo ya
mwisho.
Mfungaji bora wa fainali za 29 za AFCON, Emmanuel Emenike,
Godfrey Oboabona, John Obi Mikel na Victor Moses wanatarajia kucheza
fainali zao za kwanza za kombe la dunia.
Kikosi kizima:
Walinda mlango: Vincent Enyeama, Austin Ejide, Chigozie Agbim
Walinzi: Joseph Yobo, Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa,
Godfrey Oboabona, Azubuike Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Efe Ambrose, Kunle
Odunlami
Viungo: John Mikel Obi, Ogenyi Onazi, Ramon Azeez, Michael Uchebo, Reuben Gabriel
Washambuliaji: Osaze Odemwingie, Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Babatunde Michael, Victor Moses, Uche Nwofor. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Washambuliaji: Osaze Odemwingie, Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Babatunde Michael, Victor Moses, Uche Nwofor. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment