kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen ameongezewa mkataba wa miaka miwili, leo ametaja kikosi cha timu hiyo kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Morocco mwezi ujao kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwakani.
Katika kikosi hicho, kocha huyo Mdenmark amemuorodhesha kipa wa Yanga, Ally Mustafa ‘Barthez’ pamoja na makipa wengine watatu, Juma Kaseja wa Simba SC, Mwadini Ally na Aishi Manula wa Azam.
Upande wa mabeki amewaita Erasto Nyoni, Aggrey Morris wa Azam, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga SC, Shomary Kapombe wa Simba SC na Yahya Mudathir wa Azam.
Kwa viungo, Poulsen amewaita Haroun Chanongo, Mrisho Ngassa wa Simba SC, Simon Msuva, Frank Domayo, Athumani Iddi ‘Chuji’ wa Yanga SC, Salum Abubakar, Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Azam FC na washambuliaji ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC, John Bocco wa Azam FC, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar na Zahor Pazi wa JKT Ruvu.
Katika kikosi hicho, wameachwa wachezaji watano ambao ni mabeki Issa Rashid, Nassor wa Mtibwa, Masoud ‘Chollo’ wa Simba SC na viungo Shaaban Nditi wa Mtibwa, Amri Kiemba na Mwinyi Kazimoto wa Simba SC.
Katika kikosi hicho, wameachwa wachezaji watano ambao ni mabeki Issa Rashid, Nassor wa Mtibwa, Masoud ‘Chollo’ wa Simba SC na viungo Shaaban Nditi wa Mtibwa, Amri Kiemba na Mwinyi Kazimoto wa Simba SC.
Lakini Poulsen amesema Mwinyi atamuangalia zaidi kabla ya kuchukua uamuzi wa mwisho juu ya kumchukua au kumtema moja kwa moja.
Stars inaweza kucheza na Ethiopia Juni 2, mwaka huu kabla ya kumenyana na Morocco mjini Marakech.
Pamoja na hayo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema limeitoa timu hiyo kushiriki michuano ya nchi za Kusini mwa Afrika, COSAFA kutokana na kubanwa na ratiba ya mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia.
TFF imesema iliwaomba COSAFA warekebishe ratiba ya Stars, lakini wakagoma na kwa sababu hiyo wamejitoa.
Poulsen alianza kuinoa Stars Mei mwaka jana akitokea timu za vijana nchini, kurithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Poulsen na tangu wakati amekwishaiongoza timu hiyo katika mechi 10, akishinda tano, sare tatu na kufungwa mbil
No comments:
Post a Comment