Juhudi za uokoji zinaendelea
siku ya pili Kaskazini mashariki mwa Afghanistan ambapo watu wapatao
elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na maporomoko ya ardhi katika
maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.
Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa
wa karibu mita kumi kwenda juu baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja
kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz"Taarifa zinasema ardhi na matope yameendelea kuporomoka ambapo wengi ya waliokufa ni waokoaji ambao walikwenda kutoa msaada kwa wenzao."
Waokoaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka manusura.
Mwandishi wa BBC mjini kabul anasema kuwa eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yenye umaskini mkubwa na katika taifa maskini duniani na huenda ikachukua majuma kadhaa kabla ya serikali kubaini ukubwa wa janga hilo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment