RAIS Jakaya Kikwete amewateua Dk. Grace Puja na Innocent Sebba kuwa wabunge wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga, ilisema uteuzi huo unatokana na mamlaka aliyopewa rais na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e).
Alisema ibara hiyo, inampa mamlaka rais ya kuteua wabunge wasiozidi 10 na kwamba uteuzi wa wabunge hao ulianza Machi 20, mwaka huu. Kibanga alisema kuteuliwa kwao kumekamilisha idadi ya wabunge ambao rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kikatiba.
Alisema awali Rais Kikwete aliwateua Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Asha Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria), Saada Salum Mkuya (Waziri wa Fedha) na Janeth Mbene (Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara).
Wengine walioteuliwa awali ni Profesa Sospeter Muhongo, Shamsi Vuai Nahodha, Zakhia Meghji na Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment