Jumla ya wanafunzi 438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliohiyimu elimu ya msingi mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwakani.
Idadi hiyo ni sawa an asilimia 97 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa waandishi wa habari leo imesema
ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na mwaka jana.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year
Hata hivyo, jumla ya wanafunzi 12, 432 waliofaulu,
hawajapata nafasi ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ay sekondari
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uungufu wa majengi, hali
inayowalazimisha kusubiri chaguo la pili litakalofanyika mapema mwakani.
Jumla ya wanafunzi 808,085 walisajiliwa kufanya
mtihani wa taifa mwaka 2014 lakini ni wanafunzi 792,122 tu ndio
waliofanya mtihani, hiyo ikiwa ni asilimia 98.02% ya wanafunzi wote
waliosajiliwa.
Taarifa ya Tamisemi inaongeza kuwa wavulana
wanaongoza kwa kuchagaliwa zaidi ya wasichana ambapo jumla ya wavulana
219,964 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hiyo ikiwa ni sawa
na asilimia 97.28 ya wanafunzi wote waliochaguliwa huku wasichana
wakifikia 218,996 ambayo ni sawa asilimia 97.1 ya wanafunzi
waliochaguliwa.
No comments:
Post a Comment