Spika
wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amewashauri wanaume kutowaoa
wanawake waliokeketwa akiwataja kuwa mzigo ambao hauwezi kuijenga jamii.
Kulingana
na gazeti la daily Monitor,Spika Kadaga alitoa wito huo wakati wa
sherehe ya kitamaduni ambayo inapinga ukeketaji ilioandaliwa na mfuko wa
umoja wa mataifa unaosimamia idadi ya watu na wahisani wengine. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz''Mwanamke ambaye amekeketwa hana thamani yoyote. Achaneni na wanawake waliokwenda kukeketwa na badala yake chagueni wanawake ambao hawakukeketwa na ambao wanaweza kuimarisha jamii'',alisema Bi Kadaga.
Utamaduni huo unaojulikana kama upashaji tohara wanawake umekithiri miongoni mwa tamaduni nyingi na bara la Afrika kwa jumla na hutumiwa kumuandaa mwanamke anayeolewa ama hata kuonyesha kwamba ,mwanamke amebalehe.
Nchini Uganda ,utamaduni huo hufanyika mashariki mwa Uganda katika makabila matatu ikiwemo lile la Pokot,Sabiny na Tepeth hususan katika wilaya za Kampchorwa,Kween na Bukwo.
Bi Kadaga ambaye aliyeandamana na waziri wa maswala ya kijinsia Rukia Nakadama wote walitia sahihi ya kumaliza ukeketaji nchini Uganda.
Pia aliwaonya wazazi katika eneo hilo kukoma kuwalazimisha wanao katika ndoa za mapema na badala yake kuwataka kuwapeleka shule.
Baadhi ya wanawake waliokuwa wakitekeleza tendo hilo waliiomba serikali kulisaidia kundi la watu ambao wamewacha kuwapasha tohara wanawake. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment