Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila. PICHA|MAKTABA
Mbunge wa Kigoma Kusini
(NCCR-Mageuzi), David Kafulila ameeleza namna alivyoibua sakata la
uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow na kudokeza
kuwa kitendo cha baadhi ya watuhumiwa kugoma kujiuzulu, kinaonyesha kuna
watu zaidi wanahusika.
Kafulila (32), ambaye alikuwa akiulizia suala hilo
kila mara bungeni hadi uamuzi wa kulijadili ulipofikiwa, amesema
ataendelea kulifuatilia hadi aone mwisho wake.
Akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya ufuaji umeme baada ya Tanesco
kuingia kwenye mgogoro na Kampuni ya IPTL na suala hilo kupelekwa
mahakamani.
Kwa mujibu wa masharti ya uendeshaji wa akaunti za
escrow, fedha hizo zilitakiwa zitolewe baada ya Mahakama kutoa uamuzi
wa mgogoro huo, lakini wakati ilitaka pande hizo mbili zikutane na
kukokotoa viwango vya tozo hizo, fedha hizo zilitolewa na kulipwa kwa
mmiliki mpya wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (PAP), jambo
lililosababisha kuibuka kwa kashfa hiyo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na gazeti
hili jana, Kafulila alisema alilinasa suala hilo kwenye vyombo vya
habari na baadaye kupewa kurasa nne za maelezo ya sakata hilo, lakini
baada ya kuliingiza kwenye chombo hicho cha kutunga sheria, wabunge
wenzake waliendelea kumwongezea nyaraka hadi zikafikia kurasa 604.
“Lilikuwa ni jambo la furaha kwangu kuona kwamba
wabunge wenzangu wamenipa nyaraka nyingi pamoja na kwamba walishakuwa
nazo awali, lakini hawakuwa wametaka kuzitoa hadi nilipoingiza suala
hili bungeni,” alisema Kafulila ambaye aliingia bungeni kwa mara ya
kwanza mwaka 2010... “Nyaraka hizi zilinisaidia sana.”
Kupata ufahamu wa suala hilo kulikuwa kama bahati
kwa mbunge huyo. “Nilianza kulifahamu suala la escrow nikiwa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati nikienda Uswisi. Lilikuwa
limeandikwa katika gazeti (jina tunalo) ambalo katika ukurasa wake wa
kwanza walikuwa wamechora skendo mbalimbali za IPTL, kuanzia mwaka 1995
hadi 2014,” alisema.
Aliongeza kuwa alipotoka safari aliikuta habari
hiyo ikiwa imeandikwa kwa kina katika gazeti The Citizen na hivyo
kumfanya ajenge hamu ya kutaka kujua undani wake. Alisema alianza
kulifuatilia suala hilo kwa kuwasiliana na mmoja wa mawaziri wa Wizara
ya Nishati na Madini ambaye awali alikuwa na utaratibu wa kumjulisha
kila jambo linalofanywa na wizara hiyo.
“Nilimweleza mambo ambayo wizara inatakiwa
kuyajibu kuhusu wizi wa fedha hizo ambao unaandikwa katika magazeti.
Alinijibu kuwa wanaoandika habari hizo ni wababaishaji na wanaandika
vitu wasivyovijua,” alisema.
Alisema kutokana na unyeti wa suala hilo na sifa
walizokuwa wakipewa watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, hakukata
tamaa na kuamua kulipeleka suala hilo bungeni ili litolewe ufafanuzi wa
kina.
“Kabla ya mkutano wa Bunge kuanza nilimtafuta mtu
mmoja (anamtaja jina) ambaye alinipa kurasa nne tu kuhusu IPTL na escrow
tena kwa siri kubwa. Nilipozisoma nilielewa suala hilo. Mei mwaka huu
wakati nikichangia hotuba ya Waziri Mkuu bungeni niliibua sakata hilo na
kutaja majina ya wahusika,” alisema.
Na Mwananchi
Alisema wakati akichangia alitaka uchunguzi kuhusu suala hilo
ufanyike kwa sababu nyaraka alizokuwa nazo zilikuwa hazitoshi
kuthibitisha kosa.
“Niliwataja wanaotakiwa kutoa majibu ya suala hilo
ambao ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tanesco, Benki Kuu,
Wizara ya Fedha. Nilitaka watoe majibu maana walionekana kuhusika,”
alisema.
Wakati huo, Spika Anne Makinda alimtaka
kuwasilisha nyaraka bungeni ili suala lake lijadiliwe na mbunge huyo
alisema angewasilisha. Alisema baada ya kuibua suala hilo alianza kupata
taarifa nyingi kutoka kwa baadhi ya wabunge, baadaye alibaini kuwa
walikuwa wakilijua siku nyingi lakini hawakutaka kulisema.
“Nilipata nyaraka nyingi kutoka kurasa nne
nilitengeneza faili lenye kurasa 604. Niliipata mikataba yote pamoja na
taarifa za TRA ambazo awali sikuwa nazo. Nikapata nyaraka kutoka Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Fedha, TRA, Benki Kuu na
mikataba minne ya Tanesco ya tangu mwaka 1995. Pia nilipata barua za
mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,
Benki Kuu na Hazina.”
Alisema baada ya kupata ushahidi aliendelea
kulizungumza suala hilo kwa kujiamini zaidi na ilipofika wakati wa
hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini, alilirudisha bungeni na
kulizungumza kiundani.
Alisema katika majibu yake Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alionyesha kutolijua suala hilo.
“Mfano alisema kesi za IPTL zimekwisha na mimi
nilitoa nyaraka inayoonyesha kesi hizo zinaendelea na Tanesco waliteua
mawakili wawili kwenda kusimamia kesi Uingereza. Alikuwa hajui
anachokiongea. Aliposema fedha zile (kwenye akaunti ya escrow)
zilitolewa kutokana na hukumu, mimi nilikuwa na hukumu ambayo haikusema
fedha hizo zitoke.” Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment