Meja Jenerali Godefroid Niyombareh
amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati
maalum ya kuiokoa Burundi
Raia wa Bujumbura wakishanilia tangazo la generali Niyombareh
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu
wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa
Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi
februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani
mbali na sheria za kimataifa.
Polisi wameamrishwa kuondoka mabarabarani
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga hatua ya Rais Nkurunzinza kuwania awamu ya tatu
Maafisa wa jeshi la Burundi wanaonekana wakiweka usalama
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa
kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya
mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu
ya tatu.
Raia wanashangilia mjini Bujumbura
Waandamanaji Bujumbura
Waandamanaji Bujumbura
Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''
Raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi Bujumbura
Raia wakishangilia ''mapinduzi''
Vifaru vya kijeshi katikati ya mji mkuu Bujumbura
No comments:
Post a Comment