Atletico
Madrid imenyakua kombe la ligi kuu ya Hispania La liga baada ya kutoka
sare ya 1 – 1 dhidi ya Barcelona na hivyo kumaliza ligi ikiwa na pointi
90 huku Barcelona ikishika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 87.
Real Madrid iliyoshinda mechi yake
dhidi ya Espanyol kwa 3 - 1 ikishika nafasi ya tatu kwa kumaliza ligi
ikiwa na pointi 87 lakini ikizidiwa na Barcelona kwa tofauti ya goli
moja.
Barcelona wana tofauti ya magoli 67 wakati Real Madrid ikiwa na tofauti ya magoli 66.
Katika mechi hiyo ya Barcelona dhidi
Atletico Madrid ambayo ilikuwa ni ya kuamua ni timu ipi itanyakua ubigwa
wa La Liga msimu huu, Barcelona ndio waliokuwa wa kwanza kuutikisa wavu
wa Atletico Madrid kwa goli lililofungwa na Alexis Sanchez katika ya 34
kipindi cha kwanza.
Baadae Atletico Madrid walikuja juu na
kuanza kulishambulia goli la Barcelona ambapo Diego Godin katika dakika
ya 49 kipindi cha pili aliIsawazishia timu yake kwa goli safi
alilolipachikwa wavuni kwa njia ya kichwa na hivyo kufanya mechi hiyo
imalizike kwa jumla ya goli 1 - 1 .
Atletico Madrid inakuwa mabingwa wa La Liga tangu baada ya kulikosa kombe hilo tangu mwaka 1996. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment