Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema
aliacha kwenda uwanjani kuiangalia timu ya taifa Stars kwa kuwa
alionekana kuitia mkosi wa kufungwa timu hiyo kila ilipocheza.
Akiongea
wakati wa kuvunja bunge na kuwaaga wabunge, Rais Kikwete alisema
zamani alihudhuria sana mechi za Stars na baada ya kuonaa inafungwa mara kwa mara,
aliamua kuacha kwenda uwanjani .
“Mwanzoni nilikuwa navaa hadi jezi
kuishangilia timu yetu ilipokuwa inafanya vizuri, tulipoanza kufungwa
fungwa wakasema mzee unaitia timu mkosi, nikaamua kuacha”, alisema Rais
Kikwete huku akicheka katika hali ya mzaha.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
“Lakini hata baada ya
kutokwenda uwanjani, timu imeendelea kufungwa tu, tusikate tamaa”,
alisema Rais Kikwete mpenda michezo. Taifa Stars imetolewa michuano ya
kufuzu ya CHAN na Uganda na sasa ina kibarua cha kufuzu fainali za AFCON
mwaka 2017.
Hata
hivyo, Rais Kikwete amewataka Watanzania kutokata tamaa na kufanya
vibaya kwa sekta ya michezo na badala yake jitihada za kuendeleza sekta
hiyo ziendelee na ipo siku sekta hiyo itafanya vizuri kimataifa.
Amesema serikali yake imefufua michezo ya mashuleni ili kukuza vipaji kwa ajili ya taifa hapo baadae na pia
serikali yake imeingia ubia na makampuni ya kimataifa yay a Symbion
Power na klabu ya Sunderland ya Uingerteza kwa ajili ya kujenga kituo
cha michezo kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam ambacho kinategemewa
kuanza kazi mwezi Septemba.
“Tujitahidi, tusikate tama, tutafika
tunapopakusudia”, alisema Rais Kikwete katika hotuba hiyo ambayo
aliitumia kulianga bunge akijiandaa kuachia madaraka mwezi Oktoba mwaka
huu baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Rais na wabunge.
Rais
Kikwete amesema serikali yake pia imechukua jitihada za makusudi
kuendeleza sekta ta muziki na filamu kwa kuwaalika wataalamu kutoka
Marekani kutoa mafunzo ya sekta hizo kwa wasanii wa Tanzania ili wafanye
kazi nzuri itakayotambulika kimataifa.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
No comments:
Post a Comment