Mashoga hao wakifungishwa ndoa kwenye ofisi ya msajili nchini Uingereza.
Wanawake wawili raia wa Pakistan wameweka historia kama Waislamu wa kwanza wa jinsia moja kufunga ndoa nchini Uingereza.
Rehana
Kausar, miaka 34, na Sobia Kamar, miaka 29,wameweka historia pale
walipofunga pingu za maisha katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi ya
msajili, kisha haraka wakaomba hifadhi ya kisiasa baada ya kuwa
wamefunga ndoa, wakidai kwamba maisha yao yatakuwa hatarini kama
wakirejea kwenye nchi yao ya asili.
Wakishuhudiwa
na wasimamizi wao na marafiki wawili, wanandoa hao walivalia mavazi
meupe asilia ya ndoa pale walipofunga ndoa mjini Leeds, West Yorkshire.
Wawili
hao, kutoka mikoa ya Lahore na Mirpur ya Pakistan, walisema walipokea
vitisho vya kuuawa kutoka kwa wapinzani nchini Pakistan - ambako
mahusiano ya jinsia moja ni kinyume cha sheria na kuchukuliwa ni
kusaliti Uislamu.
Na
tangu habari za ndoa yao mapema mwezi huu kuzagaa, wanandoa hao walidai
kupokea vitisho vya kuuawa hata kutoka nchini Uingereza
Kabla
ya zoezi hilo, hata msajili aliwashauri wawili hao kufikiria kwa makini
kuhusu uamuzi wao wa kufunga ndoa sababu ya mtazamo wa baadhi ya
Waislamu kuhusu mahusiano ya jinsia moja.
Kausar alisema: "Nchi hii inatupatia uhuru wa kuamua na ni uamuzi binafsi mno ambao tumeuchukua.
"Halimuhusu mtu mwingine yeyote kwa hili tunalofanya katika maisha yetu binafsi.
"Tatizo
lililopo Pakistan ni kwamba kila mmoja anaamini ni nyapara wa maisha ya
watu wengine na anaweza kuamua vema kuhusu imani za watu wengine lakini
huo si mtazamo sahihi na tupo katika taifa hili sababu ya makasisi wetu
ambao wameteka nyara jamii yetu ambayo ni jamii vumilivu na
inayoheshimu uhuru wa watu binafsi."
Kamar, alimwelezea mpenzi wake kama 'mwenza wa kiroho' na alisema wanawake hao wawili walizama kwenye mapenzi.
Sheria za Pakistan hazitambui ndoa za jinsia moja na hakuna sheria kukomesha ubaguzi.
Wanawake wote walikutana mjini Birmingham kama wanafunzi ndipo wakahamia nchini Pakistan kutoka Uingereza.
Baadaye walianza kuishi pamoja kama wapenzi huko South Yorkshire, ambako walikaa mwaka mmoja kabla ya kuamua kufunga ndoa.
Jamaa mmoja alisema: "Wapenzi
hao hawakuwa na ndoa ya Kiislamu, inayofahamika kama 'nikah', kutokana
na kushindwa kumpata Imamu wa kuendesha kile kinachoonekana kama ndoa
yenye utata.
"Wamekuwa majasiri wakati wote kutokana na dini yetu kukataza mahusiano ya jinsia moja.
"Wanandoa hao wamekuwa wakitishiwa maisha kote hapa na Pakistan na hakuna namna yeyote wanayoweza kurejea kule."
Wanafunzi wengi wa Sharia - Sheria ya Kiislamu wanatazama mahusiano ya jinsia moja kama ni dhambi inayostahili adhabu kali.
Hakuna adhabu maalumu iliyotajwa lakini katika kesi nyingi za watu mashoga wanaopatikana na hatia huweza kuhukumiwa kifo.
No comments:
Post a Comment