Raia
nchini Pakistan wanaadhimisha siku tatu za maombolezo kuwakumbuka zaidi
ya watu 140 waliouwawa,karibia wote wakiwa watoto katika shambulio
lililotekelezwa na kundi la Taliban.
Waziri mkuu Nawaz Shariff
ameitisha mkutano wa vyama vyote vya kisiasa nchini humo kujadili vile
watakavyoweza kujibu shambulizi hilo la Peshawar.Ameelezea shambulizi hilo kuwa janga la kitaifa lililotekelezwa na wakatili.
Mkuu wa jeshi Jenarali Raheel Shariff ameahidi kulipiza kisasi kwa kila tone la damu linalomwagika.
Nchini India ,shule zimenyamaza kwa dakika mbili ili kutoa heshima kwa wale waliouawa.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment